169 – Abu Twaalib Makkiy bin ´Aliy bin ´Abdir-Razzaaq al-Hariyriy ametukhabarisha: Abu Ishaaq Ibraahiym bin Muhammad bin Yahyaa al-Muzakkaa ametuhadithia: Muhammad bin Ishaaq bin Ibraahiym ath-Thaqafiy ametuzindua: Muhammad bin Bakkaar ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Ja´far, Ibn-ul-Mubaarak, ad-Daraawardiy na ´Abdullaah bin Ja´far wametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin Sa´iyd bin Abiy Hind, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Wakati na uzima ni neema mbili wanazoghafilika kwazo watu wengi.”[1]

170 – Abul-Hasan ´Aliy bin Ahmad bin ´Umar al-Muqriy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdillaah bin Ibraahiym ash-Shaafi´iy ametuhadithia: Mu´aadh bin al-Muthannaa ametuhadithia: Musaddad ametuhadithia: ´Abdullaah bin Daawuud ametuhadithia, kutoka kwa Ja´far bin Burqaan, kutoka kwa Ziyaad bin al-Jarraah, kutoka kwa ´Amr bin Maymuun, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia bwana mmoja ambaye alikuwa akimuaidhi:

”Faidika na mambo matano kabla hujafikwa na matano: ujana wako kabla ya uzee wako, uzima wako kabla ya ugonjwa wako, utajiri wako kabla ya ufukara wako, wakati wako kabla ya kushughulika kwako, uhai wako kabla ya kifo chako.”[2]

171 – Abu Muhammad al-Hasan bin ´Aliy bin Ahmad bin Bashshaar as-Swaabuuriy ametukhabarisha huko Baswrah: Abu Bakr Muhammad bin Ahmad bin Mahmuuyah al-´Askariy ametuhadithia: Ja´far bin Muhammad al-Qalaanisiy ametuhadithia: Aadam bin Abiy Iyaas ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia: Sa´iyd al-Jariyriy ametuhadithia: Ghunaym bin Qays amesema:

”Tulikuwa tukipata mazingatio kabla ya Uislamu: ”Ee mwanadamu! Fanya matendo katika wakati wako kabla ya kazi yako, katika ujana wako kabla ya uzee wako, katika uzima wako kabla ya ugonjwa wako, katika dunia yako kwa ajili ya Aakhirah yako, katika maisha yako kwa ajili ya kifo chako.”[3]

172 – Kumehadithiwa kutoka kwa Muhammad bin ´Abdillaah, mpwa wa Maymaa, aliyesema: Ja´far bin Muhammad bin Nuswayr ametuzindua: Ahmad bin Muhammad bin Masruuq at-Twusiy ametuhadithia: Nilimsomea Mahmuud bin al-Hasan maneno yake:

Kimbilia ujana wako kabla ya kuwa kwako mzee

na uzima wa mwili wako kabla kugonjweka

na masiku ya maisha yako kabla ya kufa kwako –

ni muda kiasi gani aliye hai amebakiza kuishi?

Ukimbilie wakati wako

kabla ya nyusiku ulizoshughuliswa

Fanya matendo, kwa sababu kila mtu anasogea mbele

kwa mujibu wa yale aliyotatanguliza katika matendo

173 – Ibraahiym bin ´Umar al-Barmakiy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdillaah bin Khalaf ametuzindua: Ibn Dhariyh ametuhadithia: Hannaad bin as-Sarriy ametuhadithia: Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, aliyesema:

”Niliwasikia wakisema kwamba Shurayh aliwaona majirani zake wakiendeshwa huku na huko, kisha akawaambia: ”Mna nini?” Wakasema: ”Leo tumepata wakati.” Ndipo Shurayh akawaambia: Je, aliye na wakati anakuwa namna hiyo?”

[1] al-Bukhaariy (6412) na Ahmad (1/258).

[2] Swahiyh. Ni kweli kwamba kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi na ni nzuri, lakini Ibn Abiyd-Dunyaa katika “Qasr-ul-Amal” na al-Haakim (4/306) wote wawili wameisimulia kwa cheni za wapokezi zilizoungana kupitia njia zingine kutoka kwa Ibn ´Abbaas. al-Haakim na adh-Dhahabiy wote wawili wameisahihisha kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim, mambo ni kama walivosema.

[3] Abul-´Anbar Ghunaym bin Qays al-Maaziniy kutokea Baswrah alikuwa ni mwanafunzi wa Maswahabah. Anasimulia kutoka kwa Abu Muusa al-Ash´ariy, Sa´d bin Abiy Waqqaas na baba yake, ambaye alikuwa Swahabah. Kuna wasimulizi wengi madhubuti ambao wamesimulia kutoka kwake. Ibn Hibbaan amemtaja katika ”ath-Thiqaat” na akasema kuwa alikufa mwaka wa 90. Sa´iyd al-Jariyr hakusikia chochote kutoka kwake. Baina yao alikuweko mtu mwingine. Abu Nu´aym amepokea masimulizi hayohayo kupitia njia mbili kutoka kwa al-Jariyriy, kutoka kwa Abus-Sulayl, ambaye amesema: ”Ghunaym bin Qays amenambia… ”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 98-100
  • Imechapishwa: 26/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy