38. Msimamo wa waliozinyamazia sifa

Makundi mawili yaliyonyamaza ni:

1- Kundi ambalo linaona kwamba maandiko yanaweza kumthibitishia Allaah sifa zinazolingana Naye. Upande mwingine hawahitajii kufanya hivo. Fuqahaa´ wengi na wengineo wana mtazamo huo.

2- Kundi ambalo wamepuuzia yote hayo kikamilifu. Wametosheka peke yake na kusoma Qur-aan na Hadiyth.

Tofauti kati ya makundi haya mawili, ni kuwa hilo la kwanza linaonelea kuwa yote mawili yanawezekana; kuthibitisha sifa na kutothibitisha. Kundi la pili halisemi kitu kabisa – na Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath Rabb-il-Bariyyah, uk. 88
  • Imechapishwa: 13/05/2020