Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
20 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kusahau ilihali amefunga ambapo akala au akanywa, basi aikamilishe funga yake. Hakika si vyenginevyo Allaah ndiye kamlisha na kumnywesha.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
21 – Katika upokezi wa al-Haakim imekuja:
“Mwenye kufungua katika Ramadhaan kwa kusahau basi hakuna juu yake kulipa wala kafara.”[2]
Nayo ni Swahiyh.
MAELEZO
Hadiyth hii ni dalili kwamba mfungaji akila au kunywa kwa kusahau, basi swawm yake ni sahihi na haina upungufu wowote. Aidha hana dhambi kwa hilo, kwa sababu hakukusudia kufanya hivyo, bali ni riziki ambayo Allaah amemletea. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameihusisha kula na kunywa huku na Allaah (Ta´ala). Pia hatohitaji kulipa siku hiyo, kwa sababu ameamrishwa aitimize swawm yake na ametajwa kuwa anaendelea kufunga. Kwa hiyo ikafahamisha kuwa ni mwenye kufunga kikweli, jambo ambalo kuna maafikiano juu yake. Isipokuwa Imaam Maalik, Rabiy‘ah ar-Ra’y na Ibn Abiy Laylaa ndio ambao wanaona kwamba swawm yake imeharibika na kwamba analazimika kulipa siku hiyo, kwa sababu kujizuilia na vifunguzi ni nguzo ya swawm, kama mtu aliyesahau nguzo miongoni mwa nguzo za swalah. Maana ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”… basi aikamilishe funga yake.”
ni kwamba aendelee kujizuia na vitu vinavyobatilisha swawm hadi kufuturu. Lakini maoni sahihi ni kwamba swawm yake ni sahihi na hahitaji kulipa, kwani Hadiyth yenyewe ni hoja wazi juu ya hilo. Wengi miongoni mwa wanazuoni wa baadaye wa Maalikiyyah wamekhitilafiana na Imaam Maalik katika jambo hili. Pia imepokelewa kwamba Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kufunga akila au akanywa kwa kusahau, basi hakika hiyo ni riziki ambayo Allaah amemletea na wala hatakiwi kulipa.”[3]
Hii ni dalili ya wazi juu ya swawm yake kuwa sahihi na kutotakiwa kulipa. Hata hivyo kuna wanazuoni waliotaja kuwa tamko lisemalo:
”… wala hatakiwi kulipa.”
linapingana na Hadiyth zilizo Swahiyh.
[1] al-Bukhaariy (1933) na Muslim (1155).
[2] al-Haakim (1/430).
[3] Ibn Khuzaymah (1990), al-Daaraqutwniy (02/178), Ibn Hibbaan (08/288) na al-Haakim (01/430). al-Daaraqutwniy amesema:
“Mlolongo wake wa upokezi ni Swahiyh.”
Lakini Hadiyth iko kwa Muslim (1000) bila ya sentesi isemayo ”Wala hatakiwi kulipa.” Tazama ”Sharh ´Umdah” ya Ibn Taymiyyah.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/50-51)
- Imechapishwa: 24/02/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/50-51)
Imechapishwa: 24/02/2025
https://firqatunnajia.com/38-hadiyth-mwenye-kusahau-ilihali-amefunga/