37. Unavyofanyia wengine ndivo utavyofanyiwa, ulichopanda ndicho utachovuna

162 – ´Aliy bin Muhammad bin ´Abdillaah al-Mu-addil ametukhabarisha: al-Husayn bin Swafwaan al-Bardha´iy ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa ametuhadithia: Muhammad bin al-Husayn amenihadithia: Daawuud bin al-Muhabbar ametuhadithia, kutoka kwa Swaalih al-Murriy, kutoka kwa al-Hasan, ambaye amesema:

”Muumini huyapumzikia matendo yake aliyoyatanguliza ndani ya kaburi lake. Yakiwa ni ya kheri, basi ni kheri, na yakiwa ni ya shari, basi ni shari. Kwa ajili hiyo hakikisheni – Allaah akurehemuni – ya mnachangamkia fursa katika kipindi hiki kifupi.”

163 – Abu Bakr Muhammad bin ´Umar bin Ja´far al-Khiraqiy ametukhabarisha: Abu Bakr Ahmad bin Ja´far bin Muhammad bin Salm al-Khuttaliy ametukhabarisha: Ahmad bin ´Aliy al-Abbaar ametuhadithia: Yahyaa bin Ayyuub ametuhadithia: ´Ammaar bin Muhammad Abul-Qattwaan ametuhadithia: kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Mujaahid, aliyesema kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا الْمُفْسِدِينَ

”Na wala usisahau fungu lako katika dunia!”[1]

”Bi maana kuyafanyia kazi maisha yako kwa ajili ya Aakhirah.”

164 – Abul-Qaasim ´Abdur-Rahmaan bin Ahmad bin Ibraahiym al-Qazwiyniy ametukhabarisha: ´Aliy bin Ibraahiym bin Salamah al-Qattwaan ametukhabarisha: Abu Haatim ar-Raaziy ametuhadithia: Swuwayd – yaani Ibn Sa´iyd – amenihadithia: Abu ´Awn al-Hakam bin Sinaan ametuhadithia, kutoka kwa Maalik bin Diynaar, ambaye amesema:

”Imeandikwa katika Tawraat: ”Unavyofanyia wengine ndivo utavyofanyiwa, ulichopanda ndicho utachovuna.”[2]

165 – Abul-Husayn Ahmad bin ´Aliy bin al-Husayn at-Tannawziy ametukhabarisha: Abu Muhammad ´Ubaydullaah bin Muhammad al-Jaraadiy al-Kaatib ametuzindua: Ibn Durayd ametusomea: ´Abdur-Rahmaan – yaani mpwa wa al-Asma´iy – ametusomea, kutoka kwa ami yake: Bwana mmoja wa Baswrah ametusomea:

Kabla ya Siku ya mkusanyiko hauna kitu kingine zaidi ya

kile ulichojikusanyia kabla ya kufa kwa ajili ya Mkusanyiko

Ikiwa hujapanda na kuona mvunaji

unajuta juu ya kupuuza wakati wa kupanda

166 – Muhammad bin al-Husayn bin al-Fadhwl al-Qattwaan ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ja´far bin Darastuuyah ametukhabarisha: Ya´quub bin Sufyaan ametuhadithia: Shihaab bin ´Abbaad amedai kuwa Sufyaan alikuwa akipigia mfano kwa beti za al-A´shaa:

Ikiwa utaondoka bila ya akiba ya chakula cha uchaji Allaah

na ukakutana, baada ya kufa, na ambaye amebeba akiba ya chakula

utajuta ni kwa nini hukuwa kama yeye

na kwamba hukuona yale ambayo yeye ameona

167 – Ibraahiym bin ´Umar al-Barmakiy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdillaah bin Khalaf ad-Daqqaaq ametukhabarisha: Muhammad bin Swaalih bin Dhariyh al-´Ukbariy ametukhabarisha: Hannaad bin as-Sarriy ametuhadithia: Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa bwana mmoja, kutoka kwa al-Hasan, ambaye alikuwa akisema kunapoingia asubuhi na kunapoingia jioni:

Kijana atafurahika na ule uchaji Allaah ambao atakuwa ametanguliza

atakapojua magonjwa ambayo yatamuua

168 – Abu ´Abdillaah Muhammad bin ´Abdil-Waahid bin Muhammad bin Ja´far ametukhabarisha: Muhammad bin al-´Abbaas ametuzindua: Ahmad bin Sa´iyd as-Suusiy ametukhabarisha: ´Abbaas bin Muhammad ametuhadithia: Yahyaa bin Ma´iyn amesema katika beti moja:

Unapohitaji riziki basi hutopata

riziki ambayo ni bora zaidi kama matendo mema

Yahyaa amesema:

”Haya ni ya al-Akhtwal.”

[1] 28:77

[2] Wagalatia 6:7.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 95-97
  • Imechapishwa: 26/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy