Swali 37: Ni muda kiasi gani Mtume (Swalla Allaahu ´alyhi wa sallam) aliikaa Qubaa´?
Jibu: Kwa mujibu wa Ibn Ishaaq alikaa huko kuanzia jumatatu hadi alkhamisi. Kisha akatoka mahali hapo siku ya ijumaa. Swalah ya ijumaa ikamkuta akiwa kwa kabila la Banuu Saalim bin ´Awf. Hiyo ndio swalah ya ijumaa aliyoswali Madiynah. Kabila la ´Amr bin ´Awf wanadai kuwa alikaa muda mrefu zaidi ya huo.
- Muhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 105-106
- Imechapishwa: 03/10/2023