Kuhusu Hadiyth isemayo:
“Ajiepushe nayo mfungaji.”[1]
Abu Daawuud amesema baada yake:
“Yahyaa bin Ma‘iyn amenambia kuwa ni Hadiyth dhaifu.”
Vivyo hivyo amesema Imaam Ahmad, kama Abu Daawuud alivyonukuu kutoka kwake. Kasoro ya Hadiyth hii ni baba yake ‘Abdur-Rahmaan, naye ni an-Nu‘maan bin Ma‘bad, ambaye hatambuliki, kama ilivyotajwa katika ”at-Taqriyb” na vitabu vingine. Ama ‘Abdur-Rahmaan mwenyewe, Ibn Ma‘iyn amemdhoofisha, ingawa Abu Haatim amesema ni mkweli na Ibn Ḥibbaan amemtaja katika ”ath-Thiqaat”.
Kunatumiwa kipimo cha wanja zile matone ya jicho, kwa sababu zina maana ya wanja. Vivyo hivyo matone ya sikio, kama ilivyotangulia. Ama matone ya puani, basi yanafunguza ikiwa yatafika tumboni mwake, kwa sababu pua ni njia inayoelekea kwenye tumbo. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Laqiytw bin Swabirah:
“Fanya kishindo katika kuyapindisha maji puani isipokuwa ukiwa umefunga.”
Na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] as-Sunan (2377).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/49)
- Imechapishwa: 24/02/2025
Kuhusu Hadiyth isemayo:
“Ajiepushe nayo mfungaji.”[1]
Abu Daawuud amesema baada yake:
“Yahyaa bin Ma‘iyn amenambia kuwa ni Hadiyth dhaifu.”
Vivyo hivyo amesema Imaam Ahmad, kama Abu Daawuud alivyonukuu kutoka kwake. Kasoro ya Hadiyth hii ni baba yake ‘Abdur-Rahmaan, naye ni an-Nu‘maan bin Ma‘bad, ambaye hatambuliki, kama ilivyotajwa katika ”at-Taqriyb” na vitabu vingine. Ama ‘Abdur-Rahmaan mwenyewe, Ibn Ma‘iyn amemdhoofisha, ingawa Abu Haatim amesema ni mkweli na Ibn Ḥibbaan amemtaja katika ”ath-Thiqaat”.
Kunatumiwa kipimo cha wanja zile matone ya jicho, kwa sababu zina maana ya wanja. Vivyo hivyo matone ya sikio, kama ilivyotangulia. Ama matone ya puani, basi yanafunguza ikiwa yatafika tumboni mwake, kwa sababu pua ni njia inayoelekea kwenye tumbo. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Laqiytw bin Swabirah:
“Fanya kishindo katika kuyapindisha maji puani isipokuwa ukiwa umefunga.”
Na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] as-Sunan (2377).
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/49)
Imechapishwa: 24/02/2025
https://firqatunnajia.com/37-mfungaji-na-dawa-za-matone-ya-maji/