37. Maoni ya Ibn ´Abbaas mwanamke kuonyesha jicho moja

Muheshimiwa al-Mawduudiy amesema:

”Aayah imeteremshwa maalum kwa ajili ya kufunika uso.”[1]

Kutokana na ninavojua hakuna mwanachuoni yeyote aliyemtangulia kusema hivo. Wala mtazamo wake hautokani na dalili yoyote sahihi inayoweza kutegemewa. Isipokuwa labda atumie upokezi wa Ka´b al-Quradhwiy, lakini cheni yake ya upokezi ni nyonge sana ambayo haifai kuijengea hoja na kuitegemea. Wala si sahihi yale aliyonukuu kutoka kwa Ibn ´Abbaas pale aliposema:

”Allaah amewaamrisha wanawake wa kiumini wanapotoka majumbani mwao kwa sababu ya haja fulani wafunike nyuso zao kwa jilbaab…”

Hakuyataja kwa ukamilifu:

”… na wabakize jicho moja tu.” (Jaamiy´-ul-Bayaan)

Upokezi kutoka kwa Ibn ´Abbaas haukusihi. at-Twabaraaniy ameyapokea kupitia kwa ´Aliy bin Abiy Twalhah. Licha ya kwamba amejeruhiwa na baadhi ya maimamu, hakusikia kutoka kwa Ibn ´Abbaas, bali hakumuona. Imesemekana kuwa Mujaahid ndiye aliyekosekana baina yao. Ikiwa mambo ni hivyo basi mlolongo wa wapokezi ni wenye kuungana. Lakini katika njia kwenda kwake yuko pia Abu Swaalih ´Abdullaah bin Swaalih ambaye yuko na unyonge. Vilevile Ibn Jariyr amepokea kutoka kwa Ibn ´Abbaas maana inayoenda kinyume na haya, lakini yenyewe pia cheni yake ya wapokezi ni dhaifu. Hata hivyo nimepata njia nyigine Swahiyh inayoitia nguvu – na himdi zote njema anastahiki Allaah.

[1] al-Hijaab, uk. 366

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 88
  • Imechapishwa: 19/09/2023