37. Dalili ya kwamba Allaah anazungumza anapotaka na vile anavotaka

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ

”Na ikiwa mmoja wa washirikina akikuomba umlinde, basi mlinde mpaka asikie maneno ya Allaah.” (09:06)

أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُواْ لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلاَمَ اللّهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ

”Je, hivi mnataraji kuwa wataamini hali ya kuwa lilikuwa kundi miongoni mwao linasikia maneno ya Allaah kisha wakayapotosha baada ya kuyaelewa na hali wanajua?” (02:75)

يُرِيدُونَ أَن يُبَدِّلُوا كَلَامَ اللَّـهِ

”Wanataka kubadilisha Maneno ya Allaah.” (48:15)

وَاتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن كِتَابِ رَبِّكَ ۖ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ

”Na soma uliyoletewa Wahy katika Kitabu cha Mola wako! Hakuna awezaye kubadilisha maneno Yake.” (18:27)

إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَقُصُّ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَكْثَرَ الَّذِي هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ

”Hakika hii Qur-aan inawasimulia wana wa israaiyl mengi ambayo wao wanakhitilafiana nayo.” (27:76)

وَهَذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ مُّصَدِّقُ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ

”Na hiki Kitabu Tumekiteremsha kilichobarikiwa kinachosadikisha yale yaliyotangulia.” (06:155)

لَوْ أَنزَلْنَا هَـٰذَا الْقُرْآنَ عَلَىٰ جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُ خَاشِعًا مُّتَصَدِّعًا مِّنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ

”Lau Tungeliiteremsha hii Qur-aan juu ya mlima, basi ungeliuona unanyenyekea na wenye kupasukapasuka kutokana na kumuogopa Allaah.” (59:21)

وَإِذَا بَدَّلْنَا آيَةً مَّكَانَ آيَةٍ وَاللّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُواْ إِنَّمَا أَنتَ مُفْتَرٍ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لاَ يَعْلَمُونَ قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ لِيُثَبِّتَ الَّذِينَ آمَنُواْ وَهُدًى وَبُشْرَى لِلْمُسْلِمِينَ وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ بَشَرٌ لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ

”Na Tunapobadilisha Aayah mahala pa Aayah nyingine – na Allaah anajua anayoyateremsha, [makafiri] husema: “Hakika wewe ni mzushi!” Bali wengi wao hawajui. Sema: “Roho Takatifu [Jibriyl] ameiteremsha kutoka kwa Mola wako kwa haki ili awathibitishie walo walioamini na ni uongofu na bishara kwa waislamu.” Na hakika Sisi tunajua kwamba wanasema: “Yuko mtu anayemfundisha haya” – lugha ya huyo wanaye muelekezea ni ya kigeni na hii ni lugha ya Kiarabu cha wazi kabisa.” (16:101-103)

MAELEZO

Qur-aan imeteremshwa na Wahy ukateremka kwa Mitume (´alayhimus-Salaam). Yeye yuko juu (Jalla wa ´Alaa). Ameteremsha Kitabu Chake kutoka juu. Amesema (Ta´ala):

قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ

“Sema: “Roho Takatifu [Jibriyl] ameiteremsha kutoka kwa Mola wako kwa haki.”

Hakika Yeye (Subhaanah) yuko juu. Ameteremsha Vitabu Vyake Tawraat, Injiyl, Qur-aan na Zabuur. Vyote vimeteremshwa kutoka kwa Allaah. Yote haya ni wajibu kumthibitishia Allaah na kwamba ndio maneno ya kweli kabisa kutoka kwa viumbe Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Kadhalika inatakiwa kuamini kwamba Qur-aan ni uongofu kwa watu, kwamba ameiteremsha kwa lugha ya kiarabu na kinawasimulia wana wa israaiyl mengi ambayo walikuwa wakitofautiana. Yote haya ni haki ambayo ni wajibu kuyaamini na kuamini yale yote yaliyoelezwa na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu maneno Yake, wito Wake, Kauli Yake, uteremsho wa Kitabu Chake na Vitabu vya Mitume wengine (´alayhimus-Salaam).

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni wenye kumthibitishia Allaah sifa hizi kwa njia inayolingana na utukufu Wake. Alisema na anasema, alizungumza na anazungumza, alinong´ongeza na ananong´oneza, alizungumza kwa siri na anazungumza kwa siri pindi anapotaka na kwa namna anayotaka (Subhaanahu wa Ta´ala).

Kuhusiana na maneno ya wanafalsafa ya kwamba maneno ni ya kale ni batili. Alizungumza na anazungumza pale anapotaka. Alimzungumzisha Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku wa kupandishwa mbinguni katika wakati wake. Alimzungumzisha Mtume Wake Muusa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) katika wakati wake. Atazungumza na watu siku ya Qiyaamah katika wakati wao. Alizungumza na Aadam (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) katika wakati wake. Atazungumza na watu wa Peponi katika wakati wao. Ni Mwenye kuzungumza (Subhaanahu wa Ta´ala) siku zote pale anapotaka. Kama alivyozungumza hapo kale pia hivi sasa ni Mwenye kuzungumza. Hakuna chenye kumzuia na kufanya hivo (Jalla wa ´Alaa). Anazungumza pale anapotaka. Hutaka pale anapotaka. Huamrisha pale anapotaka. Hukataza pale anapotaka. Hakuna mwenye kumzuia kufanya hivo (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 53
  • Imechapishwa: 22/10/2024