181 – al-Hasan bin ´Aliy ametuhatidhia: Yahyaa bin Sulaymaan al-Ju´fiy ametukhabarisha: ´Amr bin ´Uthmaan al-Ju´fiy, kutoka kwa Kuufah, ametukhabarisha: Ami yangu Abu Muslim ´Ubaydullaah bin Sa´iyd, swahiba yake al-A´mash, amenihadithia, kutoka kwa Habiyb bin Abiy Thaabit, kutoka kwa Abu ´Abdir-Rahmaan as-Sulamiy, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud, ambaye amesema:

“Niliingia kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika chumba kinachofanana na kiota cha njiwa. Alikuwa amelala kwenye mkeka wa majani ambao ulikuwa umemtia alama ubavuni mwake. Nikaanza kulia ambapo kasema: “Ee ´Abdullaah! Ni kipi kinachokuliza?” Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Kisraa na Qaysar wamezungukwa na hariri na dibaji.” Ndipo akasema: ”Usilie, ee Abu ´Abdullaah!” Wao wako na dunia na sisi tuko na Aakhirah. Nina nini mimi na dunia? Mfano wangu na dunia ni kama msafiri aliyeshuka chini ya mti ili apumzike kisha akaondoka na kuuacha.”[1]

182 – Abu Mas´uud ametuhadithia: Muhammad bin al-Fadhwl ametukhabarisha, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Hilaal bin Khabbaab, kutoka kwa ´Ikrimah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Nina nini mimi na dunia? Dunia ina nini na mimi? Hakika hapana vyenginevyo mimi na dunia ni kama mpanda farasi aliyetembea siku ya kiangazi na akatafuta kivuli chini ya mti. Kisha akaondoka na kuuacha.”[2]

183 – Abu Bakr ametuhadithia: Wakiy´ametukhabarisha, kutoka kwa al-Mas´uudiy, kutoka kwa ´Amr bin Murrah, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah, kutoka kwa ´Abdullaah, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika hapana vyenginevyo mfano wangu mimi na dunia ni kama mpanda farasi aliyetafuta kivuli chini ya mti katika siku ya joto. Kisha akaondoka na kuuacha.”[3]

[1] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1812).

[2] Ahmad (2739). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (5669).

[3] Ahmad (4196).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 45-46
  • Imechapishwa: 09/07/2025