36. Matahadharisho kwa wale wenye kufuata Aayah zisizokuwa wazi

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Imepokelewa Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Ukiwaona wale wanaofuata [Aayah] zenye kutatiza, basi [mtambue kuwa] hao ndio wale ambao Allaah amewataja [katika Qur-aan]; hivyo basi tahadhari nao!”

MAELEZO

Shaykh (Rahimahu Allaah) amesema kuwa imesihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Ukiwaona wale wanaofuata [Aayah] zenye kutatiza, basi [tambue kuwa] hao ndio wale ambao Allaah amewataja [katika Qur-aan]; hivyo basi tahadhari nao!”[1]

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amejengea dalili kwa Hadiyth hii ili kuthibitisha kuwa wale wenye kufuata Aayah zisizokuwa wazi maana yake katika Qur-aan, au katika Sunnah, na kuvisha batili zao hivyo viwili, hao ndio wale ambao Allaah amewataja na kuwasifu:

فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ

“Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu hufuata zile zenye kutatiza… “

Baada ya hapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamrisha mtu kujihadhari nao ili wasikupotezeni na Njia ya Allaah kwa wao kutufanya sisi kufuata Aayah zisizokuwa wazi maana yake. Vivyo hivyo akatuamrisha kujihadhari na njia yao.

[1] al-Bukhaariy (4547) na Muslim (2665).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 57
  • Imechapishwa: 11/11/2023