35. Mapendekezo ya kumwomba Allaah ulinzi wakati wa kuswali

Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kisha mtu anasema:

أعوذُ بِٱللَّهِ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ

“Najilinda kwa Allaah kutokamana na  Shaytwaan aliyefukuzwa na kuwekwa mbali.”

Maana ya:

أعوذُ بِٱللَّهِ

“Najilinda kwa Allaah… “

bi maana ninaomba kinga na msaada Kwako, ee Allaah.

Maana ya:

مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ

“… kutokamana na  Shaytwaan aliyefukuzwa mbali.”

bi maana aliyefukuzwa na kuwekwa mbali na rehema za Allaah, kutokana na kunidhuru duniani na Aakhirah.

MAELEZO

Maneno yake:

أعوذُ بِٱللَّهِ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ

“Najilinda kwa Allaah kutokamana na  Shaytwaan aliyefukuzwa na kuwekwa mbali.”

Imependekezwa kuomba ulinzi kabla ya kuanza kusoma ndani ya swalah. Hili linafanyika katika ile Rak´ah ya kwanza peke yake kwa mujibu wa maoni sahihi. Wako wanachuoni wengine wenye kuona kuwa anatakiwa kuomba ulinzi katika kila Rak´ah[1].

Maneno yake:

Maana ya:

أعوذُ بِٱللَّهِ

“Najilinda kwa Allaah… “

bi maana ninaomba kinga na msaada Kwako, ee Allaah.

Maana ya:

مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ

“… kutokamana na  Shaytwaan… “

Ameitwa “Shaytwaan” kwa sababu ya kuasi kwake. Kinachodhihiri ni kwamba linatokana na (شطن) pindi anapowekwa mbali kutokamana na kheri na rehema. Pia kuna maoni mengine yanayosema kuwa linatokamana na (شاط) pindi anapoangamizwa na kuchomwa moto.

ٱلرَّجِيمِ

“… aliyefukuzwa mbali.”

bi maana aliyefukuzwa na kuwekwa mbali na rehema za Allaah, kutokana na kunidhuru duniani na Aakhirah.

[1] Tazama ”al-Mughniy” (01/312) na ”al-Majmuu´” (03/272).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 61
  • Imechapishwa: 09/06/2022