36. Hivi ndivo Allaah anavyopenda harufu ya mfungaji

Jengine ni kwamba nisba ya Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) kuipenda ni kama nisba ya sifa Zake zote na matendo Yake Kwake, basi upendaji huo haufanani na upendaji wa viumbe, kama ambavyo radhi Zake, ghadhabu Zake, furaha Yake, chuki Yake, mapenzi Yake na chukizo Lake hayafanani na yale ya viumbe. Kama ambavyo dhati Yake (Subhaanahu wa Ta´ala) haifanani na dhati za viumbe. Sifa Zake hazifanani na sifa zao, matendo Yake hayafanani na matendo yao. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) anapenda maneno mazuri, nayo hupaa Kwake na matedno mema huyainua juu. Upendaji huu si kama upendaji wetu.

Kisha kuifasiri hiyo haiondoi mushkila, kwani waliloliona kuwa ni mushkila kuhusu kupendezwa huko linajitokeza vilevile katika radhi. Basi akisema kuwa radhi Yake si kama ya viumbe, basi waseme pia kwamba kupendezwa Kwake si kama kupendezwa kwa viumbe. Namna hii ndivo yanatakiwa kutaamiliwa mambo yote yanayohusiana na mada hii.

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 63-64
  • Imechapishwa: 10/08/2025