Shaykh Abu ´Umar akajengea hoja kwa yale aliyoyataja Abu Haatim katika “as-Swahiyh” yake kwa kuweka kizuizi kuwa ni wakati wa kuacha kula, jambo ambalo linafahamisha kuwa inahusiana na kwamba ni duniani. Basi alipokiwekea mipaka kiwakilishi ambacho ni ”harufu ya kinywa cha mwenye swawm” kwamba ”ni bora zaidi kwa Allaah” inafahamisha kwamba ni wakati wa harufu inayotolewa. Ikiwa kiwakilishi kimewekewa sifa, hali au wakati, basi khabari yake huwa ni katika hali hiyohiyo yenye mipaka. Kwa maana nyingine ikafahamisha kuwa harufu yake ni bora zaidi mbele ya Allaah (Ta´ala) pale wakati wa kutoka kwake. Aidha amepokea al-Hassan bin Sufyaan, kutoka kwa Jaabir, ambaye amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ummah wangu umepewa katika mwezi wa Ramadhaan mambo matano… ama kuhusu jambo la pili ni kuwa wanapofika jioni, basi harufu ya vinywa vyao ni bora zaidi kwa Allaah kuliko harufu ya miski.”[1]
Kisha akataja maneno ya wafasiri wa Hadiyth kuhusu maana ya bora zaidi na kuieleza kuwa ni sifa njema kwa mwenye swawm na kuridhika kwa kitendo chake, kama walivyozoea wengi miongoni mwao kutoa tafsiri isiyo na umuhimu wowote, hata kwamba kana kwamba tafsiri hizo zimebarikiwa na zinalindwa. Hakuna dharurah yoyote ya kutoa tafsiri ya kuwa “bora zaidi mbele ya Allaah kuliko harufu ya miski” kwa maana ya sifa nzuri au kuridhika na kitendo chake na kutoka katika maana ya dhahiri ya tamko hilo. Wengi katika hawa huunda maana kwa ajili ya tamko kisha wakadai kuwa maana hiyo ndiyo iliyokusudiwa katika maandiko bila ya kuzingatia iwapo tamko hilo linatumika katika maana hiyo waliyoipanga au hapana. Ni jambo lililo wazi kuwa hilo linahusisha kutoa ushahidi juu ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa makusudio ya maneno yao ni kadhaa na kadhaa. Kama halijulikani hilo kwa kuwekwa na lugha au kwa kawaida ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kulitamka tamko hilo kwa maana hiyo au kwa kulifasiri hivyo, basi ushahidi huo ni batili. Ni jambo linalotambulika kwamba harufu nzuri bora mbele ya watu ni harufu ya miski. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akalinganisha harufu ya kinywa cha aliyefunga mbele ya Allaah (´Azza wa Jall) na uzuri wa harufu ya miski kwetu na bali ni zaidi.
[1] Shu´b-ul-Iymaan (7/211) ya al-Bayhaqiy. Dhaifu sana kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (586).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 61-63
- Imechapishwa: 10/08/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 61-63
Imechapishwa: 10/08/2025
https://firqatunnajia.com/35-harufu-bora-zaidi-kuliko-harufu-ya-miski-bila-ya-tafsiri/