Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Amesema (Ta´ala):

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا

”Na nani mkweli zaidi katika mazungumzo kuliko Allaah?” (04:87)

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا

”Na nani aliye mkweli zaidi kwa kauli kuliko Allaah?” (04:122)

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ

”Atakaposema Allaah: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam!” (05:116)

وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلً

”Na limetimia neno la Mola wako kwa kweli na uadilifu.” (06:115)

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

”Na bila shaka Allaah alimsemesha Muusa maneno kikweli.” (04:164)

وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ

“Na alipokuja Muusa katika miadi Yetu na Mola wake akamsemesha.” (07:143)

وَنَادَيْنَاهُ مِن جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا

”Na Tukamwita kutoka upande wa kulia wa mlima na tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri.” (19:52)

وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰ أَنِ ائْتِ الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

”Na [kumbuka] Mola wako alipomwita Muusa [na kumwambia]: “Nenda kwa watu madhalimu.” (26:10)

وَنَادَاهُمَا رَبُّهُمَا أَلَمْ أَنْهَكُمَا عَن تِلْكُمَا الشَّجَرَةِ

”Na Mola wao akawaita [wote wawili na kuwaambia]: “Je, kwani Mimi Sikukukatazeni mti huo.” (07:22)

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَا أَجَبْتُمُ الْمُرْسَلِينَ

”Na Siku Atakapowaita na kusema: “Mliwajibu nini Mitume?” (28:65)

MAELEZO

Aayah zote hizi tukufu ni zenye kubainisha na kuthibitisha sifa za Allaah (Jalla wa ´Alaa). Kumeshatangulia sehemu ya Aayah hizi. Hizi ni zenye kubainisha maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Allaah amesema na anasema, amezungumza na anazungumza:

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ

”Atakaposema Allaah: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam!”

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا

”Na nani aliye mkweli zaidi kwa kauli kuliko Allaah?”

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا

”Na nani mkweli zaidi katika mazungumzo kuliko Allaah?” (04:87)

يُرِيدُونَ أَن يُبَدِّلُوا كَلَامَ اللَّـهِ

”Wanataka kubadilisha maneno ya Allaah.” (48:15)

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

”Na bila shaka Allaah alimsemesha Muusa maneno kikweli.”

Aayah kuhusiana na hili ni nyingi zinazothibitisha maneno, wito na kunong´oneza:

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَا أَجَبْتُمُ الْمُرْسَلِينَ

”Na Siku Atakapowaita na kusema: “Mliwajibu nini Mitume?”

وَنَادَيْنَاهُ مِن جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا

”Na Tukamwita kutoka upande wa kulia wa mlima na tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri.” (19:52)

Hakika Yeye (Subhaanah) alizungumza na anazungumza pale anapotaka. Aliita na anaita pale anapotaka. Anamzungumzisha amtakaye katika waja Wake kama alivyomzungumzisha Muusa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) na atawazungumzisha wakazi wa Peponi. Vilevile alimzungumzisha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku aliyopandishwa mbinguni. Yote haya yalitokea. Hakika Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) anakijua kila kitu na hakuna kinachofichikana Kwake (Jalla wa ´Alaa).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 51-53
  • Imechapishwa: 22/10/2024