36. Anauliwa hali ya kuwa kafiri au hali ya kuwa muislamu?

Kikosi kikubwa cha wanazuoni wanaona kwamba kuna tofauti kati ya mwenye kuacha swalah kwa makusudi hali ya kukanusha kuwa ni wajibu. Huyu ni kafiri kwa maafikiano ya wanazuoni. Wameona pia kuwa ambaye atakubali kuwa ni wajibu, lakini hata hivyo akazembea na kuhisi uvivu kwamba ni mtenda dhambi nzito na yuko khatarini. Kwa msemo mwingine hawakumtoa katika Uislamu. Wameona kuwa mtawala wa waislamu anakiwa kumfunga gerezani, kumuadhibu na kumtaka atubie kwa muda wa siku tatu. Akitubu basi tawbah yake itakubaliwa. Akiendelea kukataa baada ya siku tatu shingo yake itakatwa[1].

Aidha wametofautiana kama atauliwa hali ya kuritadi au hali ya kusimamishiwa adhabu. Wale wanazuoni wenye kuona kuwa mwenye kuacha swalah ni kafiri kwa ujumla wameona kuwa atauliwa kwa njia ya kuritadi. Kwa msemo mwingine ameritadi nje ya Uislamu. Wale wanazuoni wenye kuona kuwa anakufuru ukafiri mkubwa pale atapokanusha kuwa ni lazima wameona kuwa atauliwa kwa njia ya adhabu; adhabu ya mwenye kuacha swalah ni kukatwa shingo yake kwa upanga au kwa nyenzo nyingine inayoua.

Nimeona kuwa Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) anaegemea katika maoni yanayosema kuwa mwenye kuacha swalah ni kafiri. Ni mamoja ameiacha kwa uzembe na kuhisi uvivu hata kama hatopinga uwajibu wake. Vivyo hivyo ndivo anavyoona Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah). Vitabu na fataawaa zao zipo ambazo zinatamka waziwazi hayo niliyoyataja.

[1] Zayd al-Madkhaliy (Rahimahu Allaah) amesema:

”Si haki ya kila mmoja kusimamisha adhabu za Kishari´ah. Isipokuwa yule aliyetawalia madaraka ya waislamu. Mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye haki ya kusimamisha adhabu kama vile ya kumuua anayeua makusudi, anakata mkono wa mwizi, anampiga bakora mzinzi ambaye hajawahi kuingia ndani ya ndoa, atampiga mawe mzinzi ambaye kishawahi kuingia ndani ya ndoa na atampiga mijeledi mtu ambaye anawatuhumu wengine machafu na mnywaji pombe. Wakati mwingine adhabu inaweza kuwa kwa njia ya kuua. Yote haya ni mambo yanayopasa mamlaka. Hakuna mwengine yeyote, hata kama ni mwanachuoni,  anayo haki ya kusimamisha adhabu si juu ya nafsi yake mwenyewe wala waja wengine isipokuwa ikiwa kama ana idhini kutoka kwa mtawala, kwa mfano mahakimu wa kidini na maafisa wa polisi. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya jambo hili.” (at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 17-18)

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 102
  • Imechapishwa: 12/05/2026