Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
“Yule mwenye kuacha swalah amekufuru. Hakuna katika matendo kitu kukiacha ni kufuru isipokuwa swalah. Mwenye kuiacha ni kafiri. Allaah amehalalisha kumuua.”
MAELEZO
Haya ni maoni ya Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) na baadhi ya wanazuoni wengine wa Salaf. Wanaona ya kwamba mwenye kuacha swalah – ni mamoja amekanusha uwajibu wake au hakukanusha – muhimu ni kuwa ameiacha pasi na udhuru ya kwamba ni kafiri aliyetoka nje ya dini. Hii ni moja ya maoni ya wanazuoni. Wamejengea hoja kwa Qur-aan na Sunnah Swahiyh.
Miongoni mwa dalili za Qur-aan ni maneno Yake Allaah (Ta´ala):
فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ
“Wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi ni ndugu zenu katika dini.”[1]
Aayah inafahamisha kuwa wasiposimamisha swalah sio ndugu wa waumini. Kwa msemo mwingine asiyekuwa ndugu wa waumini basi makafiri ndio nduguze.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ahadi ilipo baina yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yeyote atakayeiacha amekufuru.”[2]
Imaam Ahmad na wanazuoni wengine walio pamoja naye wamezichukua dalili hizi juu ya kumkufurisha mwenye kuacha swalah akifa katika hali hiyo.
Hakuna kitendo chochote ambacho Ahl-us-Sunnah wanaona kuwa kukiacha ni ukafiri isipokuwa swalah peke yake.
[1] 9:11
[2] at-Tirmidhiy (2621), Ibn Maajah (1079) na an-Nasaa´iy (463). Ni Swahiyh kwa mujibu wa Shaykh al-Albaaniy.
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 101-102
- Imechapishwa: 12/05/2026
Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
“Yule mwenye kuacha swalah amekufuru. Hakuna katika matendo kitu kukiacha ni kufuru isipokuwa swalah. Mwenye kuiacha ni kafiri. Allaah amehalalisha kumuua.”
MAELEZO
Haya ni maoni ya Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) na baadhi ya wanazuoni wengine wa Salaf. Wanaona ya kwamba mwenye kuacha swalah – ni mamoja amekanusha uwajibu wake au hakukanusha – muhimu ni kuwa ameiacha pasi na udhuru ya kwamba ni kafiri aliyetoka nje ya dini. Hii ni moja ya maoni ya wanazuoni. Wamejengea hoja kwa Qur-aan na Sunnah Swahiyh.
Miongoni mwa dalili za Qur-aan ni maneno Yake Allaah (Ta´ala):
فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ
“Wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi ni ndugu zenu katika dini.”[1]
Aayah inafahamisha kuwa wasiposimamisha swalah sio ndugu wa waumini. Kwa msemo mwingine asiyekuwa ndugu wa waumini basi makafiri ndio nduguze.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ahadi ilipo baina yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yeyote atakayeiacha amekufuru.”[2]
Imaam Ahmad na wanazuoni wengine walio pamoja naye wamezichukua dalili hizi juu ya kumkufurisha mwenye kuacha swalah akifa katika hali hiyo.
Hakuna kitendo chochote ambacho Ahl-us-Sunnah wanaona kuwa kukiacha ni ukafiri isipokuwa swalah peke yake.
[1] 9:11
[2] at-Tirmidhiy (2621), Ibn Maajah (1079) na an-Nasaa´iy (463). Ni Swahiyh kwa mujibu wa Shaykh al-Albaaniy.
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 101-102
Imechapishwa: 12/05/2026
https://firqatunnajia.com/35-ukafiri-wa-mwenye-kuacha-swalah/