Pengine ukasema kuwa al-Qaasim ametaja kwamba ”Ibn Khuzaymah ana sharti katika ”as-Swahiyh” yake; ikiwa litatimizwa basi hupatikana usahihi na vinginevyo haisihi”. Ibn Hajar amelieleza hilo, nalo ni kwamba asiitaje kwanza Hadiyth kwa mfumo wa cheni ya wapokezi iliyopungua, akifanya hivyo basi si katika sharti lake hata kama baadaye ataitaja kwa cheni ya wapokezi iliyo kamili – hivyo inawezekana aliitaja kwa namna hiyo. Ni kweli kwamba ikiwa al-Qaasim amebainisha dosari hii katika Hadiyth hii na akataja kwamba aliitaja kwanza kwa mfumo wa cheni ya wapokezi iliyopungua, basi hayo ni maneno yanayosikilizwa. Na ikiwa hakubainisha, basi inafahamika kwamba dosari hiyo haimo ndani yake, kwani lau ingekuwapo basi angeitaja. Vipi aiache ilihali kitabu chake hakikuandikwa isipokuwa kwa ajili ya kutia nguvu dalili za madhehebu yake na kuzifanya dhaifu dalili za mpinzani? Ama uwezekano unaotokana na bila dalili, basi huo hauathiri usahihi wa kujengea hoja, kama ilivyokubalika katika msingi kwa watu wa uhakiki na ukamilifu.
31- Haafidhw Ibn Hajar ameijengea hoja kwayo na akaipinga kwa yale yanayoikhilafu. Lau kungelikuwa na dosari hiyo, basi angeibainisha. Ni jambo liko mbali kwa imamu huyu muhakiki na mwadilifu kuacha kubainisha huku akijua kwa ajili tu ya kutetea madhehebu yake.
Kutokana na yaliyotangulia imethibiti kwamba kuweka mikono juu ya kifua ndani ya swalah kuna asili iliyo thabiti na dalili kubwa. Hivyo basi haifai kwa waumini kujiepusha na jambo hilo. Vipi muislamu ajiepushe na jambo lililothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam),ambaye amesema:
“Haamini mmoja wenu mpaka matamanio yake yafuatane na yale niliyokuja nayo.”[1]?
Bali inampasa yule mwenye kumfuata (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) afanye hivyo ijapo ni katika baadhi ya nyakati.
Ee Allaah! Tuongoze katika haki ambayo watu wamekhitalifiana ndani yake – kwani hakika Wewe humuongoza unayemtaka katika njia iliyonyooka.
[1] Ibn Abiy ´Aaswim (15). Nzuri na Swahiyh kwa mujibu wa an-Nawawiy katika “al-Arba´uun an-Nawawiyyah” (41). Cheni ya wapokezi ni dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwilaal-ul-Jannah” (15).
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Hayaah as-Sindiy (afk. 1163)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fath-ul-Ghafuur fiy Wadhw´-il-Aydiy ´alaas-Suduur, uk. 65-68
- Imechapishwa: 12/05/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Hayaah as-Sindiy (afk. 1163)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fath-ul-Ghafuur fiy Wadhw´-il-Aydiy ´alaas-Suduur, uk. 65-68
Imechapishwa: 12/05/2026
https://firqatunnajia.com/07-kwa-ajili-hiyo-muumini-anapaswa-kuweka-mikono-juu-ya-kifua/