Swali 35: Ni ipi hukumu ya kucheza karata katika Ramadhaan?
Jibu: Kujishughulisha na mambo ya upuuzi ni haramu mbali na Ramadhaan na ni khatari zaidi katika Ramadhaan. Mwenye kunyimwa fadhila za mwezi huu hakika huyo ni mkhasirikaji mkubwa. Wenye kutumia nyusiku zao katika kucheza karata na mfano wa upotezaji muda mwingine kama televisheni ni mwenye kunyimwa kheri nyingi. Je, kusoma Qur-aan, kuswali swalah za Sunnah, kutafuta elimu na kukaa na watu wema hakutoshelezi? Watu hawa wanatakiwa wamche Allaah.
Mabarobaro wanaotoka na kucheza kuanzia 20:00 mpaka 04:00 wanatumia masaa nane katika michezo. Wanajiweka wenyewe katika madhambi na maneno mabaya. Huu ni upuuzi mbaya.
Jambo la pili sisi wote tuna majukumu kwa wale walio chini yetu. Baba mwenye kutoka nyumbani na kuwaacha watoto wake wanalala ni mwenye jukumu kwao. Ni wajibu kwake kuwafanyisha mazoezi watoto wake katika kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), kuwaamsha katika swalah, kuwafanya watende matendo mema na kuwafunza ukomavu. Huenda Allaah akamnufaisha kwa hilo.
Tukiwaacha watoto wakatoka na kwenda watakapo na wakarudi nyumbani pasi na kuswali, haina shaka kwamba yule mkubwa ndiye mwenye kubeba majukumu makubwa kwa hilo. Yule mkubwa anatakiwa kumcha Allaah juu ya wale walio chini yake. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا
“Enyi mlioamini! Zikingeni nafsi zenu na ahli zenu kutokamana na Moto.” (66:06)
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Nyote ni wachungaji na nyote mtaulizwa juu ya kile mlichokichunga. Mwanaume ni mchungaji kwa familia yake na ataulizwa juu yao. Mwanamke ni mchungaji na ataulizwa juu ya nyumba ya mumewe.”[1]
Sisi wakubwa iwapo tutaapuuza wachungwa wetu na tukaacha majukumu yetu, basi Allaah atatuuliza juu ya hilo. Hakika sisi tunaogopa adhabu ya Allaah (´Azza wa Jall).
Jambo la tatu tunatakiwa kusadiana katika wema na uchaji Allaah. Ukimuona mtu watoto wake wanaenda vibaya, anawapuuza na hawafunzi, hawaamrishi mema na kuwakataza maovu, basi unalazimika kumzindua juu ya hilo. Haya ndio wayawezayo. Wanaweza kuzungumza, kunasihi na kuwaelekeza waja wa Allaah.
[1] al-Bukhaariy (7138) na Muslim (1829).
- Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 48-51
- Imechapishwa: 12/06/2017

Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 48-51
Imechapishwa: 12/06/2017
https://firqatunnajia.com/35-ni-ipi-hukumu-ya-kucheza-karata-katika-ramadhaan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)