Swali 35: Tunaomba maelezo ya kina kuhusu suala la kupewa udhuru kwa sababu ya ujinga?
Jibu: Suala la kupewa udhuru kwa sababu ya ujinga limebainishwa na (Rahimahumu Allaah) na Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amelipambanua katika kitabu ”Twariyq-ul-Hijratayn na katika ”al-Kaafiyah ash-Shaafiyah”. Pia limetajwa na maimamu wa ulinganizi kama vile Shaykh ´Abdullaah Abaa Butwayn na wengineo. Vilevile Ibn Abiyl-‘Izz ametaja kitu katika hayo katika ”Sharh at-Twahaawiyyah”. Kwa kifupi ni kwamba jambo hili linahitaji maelezo. Mjinga ambaye anaweza kuuliza na kupata elimu si mwenye kupewa udhuru, kwa sababu ni lazima ajifunze, atafiti na kuuliza. Mtu mjinga anayetaka haki si kama yule mjinga asiyetaka haki. Kwa maana nyingine kuna aina mbili za wajinga:
1 – Mjinga anayeitaka haki.
2 – Mjinga ambaye haitaki haki.
Asiyeitaka haki si mwenye kupewa udhuru hata kama hawezi kupata elimu, kwa sababu haitaki haki. Lakini yule anayetaka kuijua haki, ikiwa atatafuta haki na asiifikie, basi ni mwenye kupewa udhuru. Kwa kifupi ni kwamba mjinga ambaye anaweza kuuliza na asifanye hivo, au anaweza kujifunza na asifanye hivo, si mwenye kupewa udhuru. Wajinga ambao hawawezi kujifunza wamegawanyika makundi mawili:
1 – Mjinga asiyeitaka haki, ambaye hapewi udhuru.
2 – Mjinga ambaye anaitaki haki na akaitafuta na asiifikie, huyo ni mwenye kupewa udhuru. Allaah ndiye mjuzi zaidi.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 73
- Imechapishwa: 09/01/2026
Swali 35: Tunaomba maelezo ya kina kuhusu suala la kupewa udhuru kwa sababu ya ujinga?
Jibu: Suala la kupewa udhuru kwa sababu ya ujinga limebainishwa na (Rahimahumu Allaah) na Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amelipambanua katika kitabu ”Twariyq-ul-Hijratayn na katika ”al-Kaafiyah ash-Shaafiyah”. Pia limetajwa na maimamu wa ulinganizi kama vile Shaykh ´Abdullaah Abaa Butwayn na wengineo. Vilevile Ibn Abiyl-‘Izz ametaja kitu katika hayo katika ”Sharh at-Twahaawiyyah”. Kwa kifupi ni kwamba jambo hili linahitaji maelezo. Mjinga ambaye anaweza kuuliza na kupata elimu si mwenye kupewa udhuru, kwa sababu ni lazima ajifunze, atafiti na kuuliza. Mtu mjinga anayetaka haki si kama yule mjinga asiyetaka haki. Kwa maana nyingine kuna aina mbili za wajinga:
1 – Mjinga anayeitaka haki.
2 – Mjinga ambaye haitaki haki.
Asiyeitaka haki si mwenye kupewa udhuru hata kama hawezi kupata elimu, kwa sababu haitaki haki. Lakini yule anayetaka kuijua haki, ikiwa atatafuta haki na asiifikie, basi ni mwenye kupewa udhuru. Kwa kifupi ni kwamba mjinga ambaye anaweza kuuliza na asifanye hivo, au anaweza kujifunza na asifanye hivo, si mwenye kupewa udhuru. Wajinga ambao hawawezi kujifunza wamegawanyika makundi mawili:
1 – Mjinga asiyeitaka haki, ambaye hapewi udhuru.
2 – Mjinga ambaye anaitaki haki na akaitafuta na asiifikie, huyo ni mwenye kupewa udhuru. Allaah ndiye mjuzi zaidi.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 73
Imechapishwa: 09/01/2026
https://firqatunnajia.com/35-mjinga-anayepewa-udhuru-na-asiyepewa-udhuru/