Suala la kupiga chuku linazalisha suala jengine ambalo ni kuchukua damu kwa ajili ya kufanya kipimo. Kwa mujibu wa maoni yanayosema kuwa kuumikwa kunaharibu swawm, basi kuchukua damu nyingi kwa ajili ya kufanya kipimo kunaharibu swawm. Hata hivyo haidhuru ikiwa ni kiasi kidogo. Lakini kwa mujibu wa maoni yanayosema kuwa kuumikwa hakuharibu swawm, basi kuchukua damu hakubatilishi swawm, ni mamoja damu hiyo ni nyingi au kidogo.
Kuhusu kutokwa na damu kwa bahati mbaya, kama vile kutokwa na damu puani, kutoka damu kwenye donda au kwenye jino ikiwa hajaimeza, mambo hayo hayaiharibu swawm kabisa. Ni mamoja iwe damu ni nyingi au kidogo, kwa sababu imetoka bila kutaka kwake. Msingi wa swawm ni sahihi isipokuwa kwa dalili sahihi inayothibitisha kuharibika kwake – na Allaah ndiye anajua zaidi.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/46)
- Imechapishwa: 19/02/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)