Hakika si vyenginevyo mlango huu umejengeka juu ya kuamini na kuisadikisha Qur-aan na Sunnah. Allaah (Ta´ala)  ameumba uhusiano wa kidugu usioshikika ili utumike kama mafungamano baina ya jamaa. Wakati ulipojikinga kwa Allaah kutokana na kukata udugu, Allaah akaumbia:

”Je, huridhiki kwamba namuunga yule anayekuunga, na namkata yule anayekukata?”[1]

Allaah (Ta´ala) amesema:

سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ

”Vimemsabihi Allaah vilivyomo katika mbingu na ardhi; Naye ni Mwenye nguvu Aliyeshinda, Mwenye hekima wa yote.”[2]

تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ

“Zinamsabihi mbingu saba na ardhi na vilivyomo ndani yake na hakuna kitu chochote isipokuwa kinamtukuza kwa himdi Zake.”[3]

Kuna dalili nyingi juu ya hilo ndani ya Qur-aan na Sunnah. Mnyenyekee Mola wako, kisadikishe Kitabu Chake na mwamini Mtume Wako (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ

”Basi msimpigie mifano Allaah.”[4]

Usifanye papara ya kurudisha nyuma haki kwa tafsiri zisizowezekana, kama wanavofanya mabwanyenye wa Mu´tazilah.

Vilevile matendo mema ndio chanzo. Vyanzo sio vitu vyenye miili, lakini Allaah akitaka, basi anaweza kuzifanya vikawa na miili ambapo matendo yakajionyesha kwa umbile la mtu mzuri ambayo yakamliwaza mwenye nayo ndani ya kaburi lake. Yule ambaye ataiacha Qur-aan na Sunnah ihukumu akili yake, basi amefuzu. Na yule atakayeingia katika kukengeusha, kupindisha maana na kulinganisha, basi ameitia dini yake khatarini. Na yule mwenye kunyamaza na akategemeza, basi amesalimika. Allaah anamwongoza amtakaye katika njia ilionyooka.

[1] al-Bukhaariy (4830) na Muslim (2554).

[2] 57:1

[3] 17:44

[4] 16:74

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 166-167
  • Imechapishwa: 12/06/2024