Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
Allaah (Ta´ala) amesema:
هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاء وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ
”Yeye ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi. Anajua yanayoingia ardhini na yatokayo humo na yanayoteremka kutoka mbinguni na yanayopanda humo. Naye yupamoja nanyi popote mlipo, na Allaah kwa myatendayo ni Mwenye kuyaona.” (57:04)
مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَى ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَى مِن ذَلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ
”Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao, na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao, na wala [hauwi mnong’ono wa] chini kuliko ya hivyo, na wala wa wengi zaidi isipokuwa Yeye Yu pamoja nao popote watakapokuwa, kisha Atawajulisha kwa yale [yote] waliyoyatenda Siku ya Qiyaamah. Hakika Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi daima.” (58:07)
لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا
“Usihuzunike – Hakika Allaah yupamoja nasi!” (09:40)
لَا تَخَافَا إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَى
”Msikhofu! Hakika Mimi niko pamoja nanyi; nasikia na naona.” (20:46)
إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ
”Hakika Allaah yupamoja na wenye kumcha na wale ambao wanafanya wema.” (16:128)
وَاصْبِرُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ
”Na subirini! Hakika Allaah yupamoja na wanaosubiri.” (08:46)
كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ
“Makundi mangapi machache yameshinda makundi mengi kwa idhini ya Allaah! Na Allaah yupamoja na wenye kusubiri.” (02:249)
MAELEZO
Aayah za sehemu ya mwisho zote zinazungumzia upamoja ambao ni wa kimaalum na upamoja ulioenea. Amesema (Ta´ala):

”Yeye ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi. Anajua yanayoingia ardhini na yatokayo humo na yanayoteremka kutoka mbinguni na yanayopanda humo. Naye yupamoja nanyi popote mlipo, na Allaah kwa myatendayo ni Mwenye kuyaona.”
Yeye (Jalla wa ´Alaa) anakijua kila kitu kilicho mbinguni na ardhini, kilichopita na kitakachokuja mbele. Yote hayo anayajua. Pamoja na hivyo Yeye anakuwa pamoja na waja Wake popote wanapokuwa. Bi maana anakuwa pamoja nao kwa ujuzi Wake na wakati huohuo yuko juu ya ´Arshi. Anakuwa pamoja nao kwa ujuzi Wake wenye kuwazunguka usiyofichikana na kitu. Amesema (Ta´ala):
لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا
“… ili mjue kwamba Allaah juu ya kila kitu ni Muweza na kwamba Allaah Amekwishakizunguka kila kitu kwa ujuzi Wake.” (65:12)
إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ
“Hakika Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.” (08:75)

”Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao, na wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao, na wala [hauwi mnong’ono wa] chini kuliko ya hivyo, na wala wa wengi zaidi isipokuwa Yeye Yu pamoja nao popote watakapokuwa, kisha Atawajulisha kwa yale [yote] waliyoyatenda Siku ya Qiyaamah. Hakika Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi daima.”
Ameianza na kuimalizia Aayah hii kwa ujuzi kwa lengo ili msomaji na msikilizaji ajue kuwa kinachokusudiwa ni elimu na wakati huohuo yuko juu ya ´Arshi (Jalla wa ´Alaa) na kwamba hakijifichi Kwake (Jalla wa ´Alaa) chochote.
Hali kadhalika inahusiana na upamoja wa kimaalum:
لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا
“Usihuzunike – Hakika Allaah yupamoja nasi!”
Haya yalisemwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) wakati walipokuwa pangoni. Amesema (Ta´ala) kumwambia Muusa na Haaruun (´alayhimaas-Salaam):

”Msikhofu! Hakika Mimi niko pamoja nanyi; nasikia na naona.”
Vilevile amesema (Ta´ala):

”Na subirini! Hakika Allaah yupamoja na wanaosubiri.”

“Makundi mangapi machache yameshinda makundi mengi kwa idhini ya Allaah! Na Allaah yupamoja na wenye kusubiri.”
Aayah zote hizi ni zenye kufahamisha upamoja ambao ni maalum ambapo anakuwa pamoja na mawalii Wake, wenye kumtii na Mitume Yake kwa kuwazunguka kiujuzi, kinusura na kuwatia nguvu.
Ama kuhusu upamoja wa kijumla unahusiana na kukizunguka kila kitu kiujuzi na kwamba hafichikani na chenye kufichikana na kwamba Yeye ndiye mwenye kuwaendesha na kuwapeleka.
Upamoja wa kimaalum unakuwa na ujuzi pamoja vilevile na kuwanusuru mawalii Wake na kuwatetea. Kama Alivyosema kupitia ndimi ya Mtume Wake alipomwambia Swahabah wake pindi walipokuwa pangoni:

Akamwambia Muusa na Haaruun (´alayhimaas-Salaam) walipokuwa mbele ya Fir´awn. Allaah aliwakinga kutokana na shari yake:

Hali kadhalika viumbe wote Yuko pamoja nao kwa ujuzi Wake inayokijua kila kitu. Anazijua siri zao na yale wanayonong´onezana na wakati huohuo yuko juu ya ´Arshi. Ujuzi Wake umekizunguka kila kitu. Anajua na kuona mdudu mchungu mweusi katika usiku wenye giza kingi. Anajua jinsi yanavyoenda maji ya mito na bahari na vilivyo ndani yavyo. Anajua vyote vilivyomo chini ya ardhi na vinavyohadithiwa na mioyo. Vyote hivyo hakuna kinachofichikana Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala). Amesema (Jalla wa ´Alaa):
وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ
“Na hushughuliki katika jambo lolote na wala husomi humo chochote katika Qur-aan, na wala hamtendi ‘amali yoyote isipokuwa Tunakuwa Mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo.” (10:61)
إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ
“Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Mwenye kushuhudia.” (22:17)

“… ili mjue kwamba Allaah juu ya kila kitu ni Muweza na kwamba Allaah Amekwishakizunguka kila kitu kwa ujuzi Wake.”
إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ
“Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Mjuzi.” (08:75)
وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ
“Na mwanamke yeyote yule habebi mimba na wala hazai isipokuwa kwa ujuzi Wake.” (35:11)
Elimu Yake imewazunguka viumbe. Ujuzi Wake maalum uko pamoja na mawalii Wake. Anazijua hali za viumbe Wake maalum na wengineo. Anayajua yatayokuja katika zama za mwisho. Anayajua yatayokuja siku ya Qiyaamah. Anayajua yaliyopita katika zama za kale. Yote hayo anayajua. Bali anayajua na ameyazunguka (Jalla wa ´Alaa). Kwa hiyo ni wajibu kumthibitishia nayo (Subhaanahu wa Ta´ala) na sambamba na hilo kumtakasa kushabihiana na viumbe Vyake kwenye chochote katika sifa Zake (Jalla wa ´Alaa). Haya ndio maoni ya watu wa haki ambao ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 48-50
- Imechapishwa: 22/10/2024

Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 48-50
Imechapishwa: 22/10/2024
https://firqatunnajia.com/35-dalili-ya-allaah-kuwa-pamoja-na-viumbe/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)