Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

57 – Hata hivyo haihitajii ´Arshi na vyenginevyo.

MAELEZO

Ibn Abiyl-´Izz al-Hanafiy (Rahimahu Allaah) amesema:

”Hakika mambo yalivyo ni kwamba kilichomfanya Shaykh (Rahimahu Allahah) kutaja maneno hayo hapa ni kuwa pale alipotaja ´Arshi na Kursiy ndipo akataja baada yake kutohitaji Kwake ´Arshi na kilichoko chini ya ´Arshi ili kubainisha kuwa kuumba Kwake ´Arshi na akalingana juu Yake sio kwa sababu ya kuihitaji. Amelingana juu yake kutokana na hekima iliyopelekea kufanya hivo. Kitu kuwepo juu zaidi ya kile kilicho chini hakuna maana kwamba kilichoko chini kinakizunguka kilicho juu, inakizunguka na kukibeba kile kilichoko juu. Wala haina maana kwamba kile kilichoko juu kinahitaji kile kilichoko chini. Zitazame mbingu! Ziko juu ya ardhi pasi na kuihitajia. Hali Yake Mola (Subhaanah) ni kubwa na tukufu zaidi ujuu Wake uhitajie mambo hayo! Bali yale yanayopelekea ujuu Wake ni katika mambo maalum Kwake; kwa uwezo Wake anakibeba kile kilichoko chini, anakifanya kile kilichoko chini kumuhitaji ilihali Yeye (Subhaanah) hakihitaji kilichoko chini na pia Anakizunguka. Kwa hiyo Yeye yuko juu ya ´Arshi sambamba na hilo anaizuia na kuibeba ´Arshi kwa uwezo Wake. Si Mwenye kuihitaji ´Arshi, ´Arshi ndio inayomuhitaji. Ni Mwenye kuizunguka ´Arshi, ´Arshi haimzunguki Yeye. Anaifupisha ´Arshi, ´Arshi haimfupishi Yeye. Malazimisho haya hayapatikani kwa kiumbe.

Endapo wale Mu´attwilah wanaokanusha ujuu wangelipambanua suala hili kwa upambanuzi huu, basi wangeliongozwa katika njia ilionyooka, wangelitambua kuwa akili ni yenye kuafikiana na Uteremsho na wangelifuata mwongozo wa dalili. Lakini wameacha dalili na hivyo wakashika njia isiyokuwa ya sawa. Mambo yalivo ni kama alivosema Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) wakati alipoambiwa:

”Ee Abu ´Abdillaah!

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

Amelingana vipi?” Akasema: ”Kulingana kunatambulika. Namna haitambuliki.”[2]

[1] 20:5

[2] Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 372

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 52-53
  • Imechapishwa: 29/09/2024