34. Mtu anayekutajeni mbele ya Allaah

32 – an-Nu´maan bin Bashiyr ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika miongoni mwa dhikr mnazodhukuru katika utukufu wa Allaah ni pamoja na Tasbiyh, Tahmiyd na Tahliyl. Zinaizunguka ´Arshi, wana mlio kama mlio wa nyuki na zinamtaja yule mwenye kuwataja. Je, hivi hapendi mmoja wenu siku zote akawepo mtu kwa Mwingi wa huruma anayekutajeni juu ya hilo?”[1]

[1] Hadiyth ni Swahiyh. Ameipokea Ibn Maajah (3809) na al-Haakim (1/503) ambaye amesema:

“Hadiyth ni Swahiyh juu ya sharti za Muslim.”

adh-Dhahabiy ameafikiana naye.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 96
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy