Shaykh Abu Muhammad amejengea hoja kwa Hadiyth inayoweka kizuizi cha harufu nzuri siku ya Qiyaamah. Kinachotilia nguvu maoni yake ni Hadiyth isemayo:
“Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mkononi Mwake! Hakuna yeyote mwenye kujeruhiwa kwa ajili ya Allaah, na Allaah pekee ndiye anayejua ni nani anayejeruhiwa kwa ajili Yake, isipokuwa atakuja siku ya Qiyaamah huku jeraha lake linatoa damu: rangi yake ni rangi ya damu na harufu yake ni harufu ya miski.”[1]
Basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alieleza kuhusu harufu ya jeraha la aliyejeruhiwa kwa ajili ya Allaah kuwa ni kama harufu ya miski siku ya Qiyaamah. Hii ni mithili ya alivyotoa khabari kuhusu harufu ya kinywa cha mwenye swawm. Akili ya kawaida inajulisha ya kwamba hii ni damu duniani na ile ni harufu ya kinywa, lakini Allaah (Ta´ala) anaifanya harufu ya hiki na kile kuwa ni kama miski siku ya Qiyaamah.
[1] al-Bukhaariy (5213) na Muslim (1876).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 60-61
- Imechapishwa: 09/08/2025
Shaykh Abu Muhammad amejengea hoja kwa Hadiyth inayoweka kizuizi cha harufu nzuri siku ya Qiyaamah. Kinachotilia nguvu maoni yake ni Hadiyth isemayo:
“Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mkononi Mwake! Hakuna yeyote mwenye kujeruhiwa kwa ajili ya Allaah, na Allaah pekee ndiye anayejua ni nani anayejeruhiwa kwa ajili Yake, isipokuwa atakuja siku ya Qiyaamah huku jeraha lake linatoa damu: rangi yake ni rangi ya damu na harufu yake ni harufu ya miski.”[1]
Basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alieleza kuhusu harufu ya jeraha la aliyejeruhiwa kwa ajili ya Allaah kuwa ni kama harufu ya miski siku ya Qiyaamah. Hii ni mithili ya alivyotoa khabari kuhusu harufu ya kinywa cha mwenye swawm. Akili ya kawaida inajulisha ya kwamba hii ni damu duniani na ile ni harufu ya kinywa, lakini Allaah (Ta´ala) anaifanya harufu ya hiki na kile kuwa ni kama miski siku ya Qiyaamah.
[1] al-Bukhaariy (5213) na Muslim (1876).
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 60-61
Imechapishwa: 09/08/2025
https://firqatunnajia.com/34-harufu-nzuri-zaidi-kuliko-harufu-ya-miski-siku-ya-qiyaamah/