Haafidhw al-Khatwiyb (Rahimahu Allaah) amezungumza vizuri pale alipowaraddi watu wa maoni (أهل الرأي) na kusema:

“Naapa kwamba Sunnah na njia za haki mara nyingi huja kinyume na rai na kwenda kinyume nayo kwa tofauti kubwa. Kwa hivyo waislamu hawana njia nyingine isipokuwa kuifuata na kujisalimisha nayo. Kwa sababu hii wanazuoni na watu wa dini walijiepusha na maoni na walitambua upungufu wake na khatari yake, kwa kuwa haki mara nyingi huja kinyume na maoni katika nyanja nyingi. Miongoni mwa mifano hiyo ni kukatwa vidole vya mkono ni kama kukatwa mkono kutoka begani na hivyo fidia yake ni dirhamu 6000.

Kukatwa mguu katika sehemu isiyo na madhara makubwa ni sawa na kukatwa mguu kutoka kwenye nyonga na hivyo fidia yake ni dirhamu 6000.

Kung’olewa macho yote mawili ni sawa na kukatwa ncha za masikio na hivyo fidia yake ni dirhamu 12 000.

Ikiwa mtu atapata majeraha mawili madogo kwenye kichwa basi fidia yake ni dinari 200, hata kama ngozi kati ya majeraha hayo ni salama. Lakini kama akiumizwa kati ya majeraha hayo hadi yakawa jeraha moja kubwa, ambalo lina madhara makubwa zaidi, basi fidia yake inakuwa dinari 50.

Mwanamke mwenye hedhi anatakiwa kulipa swawm yake, lakini hatolipa swalah yake.

Wanaume wawili ambapo mmoja akikatwa masikio yake yote mawili anastahili fidia ya dirhamu 12 000, lakini mwingine akiuawa na kupoteza masikio yake, macho yake, mikono yake, miguu yake na roho yake, bado fidia yake ni ileile – 12 000 – sawa na yule aliyekatwa tu ncha za masikio yake.

Kuna mifano mingine mingi kama hiyo. Je, waislamu wamepata njia yoyote nyingine isipokuwa kufuata hukumu hizo? Je, ni zipi kati ya hukumu hizi zinazolingana na rai au kufikiwa kwa kufikirika?”[1]

Katika kitabu cha Abu Muhammad bin Hazm (Rahimahu Allaah) “al-Ihkaam fiy Usuwl-il-Ahkaam” kuna mengi mazuri mfano wa haya. Hivyo basi napendekeza kwa yule anayetafuta haki kukisoma.

Mpaka hapa ndio mwisho. Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, jamaa zake na Maswahabah wote.

[1] al-Faqiyh wal-Mutafaqqih (1/152).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 24/06/2025