Wapiga ramgi ni yule ambaye anajidai kuyajua mambo yaliyofichikana, lakini sio kwa njia ya mashaytwaan, isipokuwa inakuwa kwa njia ya kubahatisha na dhana. Kwa msemo mwingine akasema kuwa pengine kukatokea mambo fulani kutokana na utabiri wa uwongo. Wanazuoni wengine wamesema kuwa mpiga ramli ndiye huyohuyo kuhani, kila mmoja katika wao anasimulia mambo yaliyofichikana lakini kwa kutumia njia mbalimbali. Ni lazima kwa muislamu kuwazingatia makuhani na wapiga ramli kuwa ni makafiri na wala asiwasadikishe. Sio katika mawalii wa Allaah, hakika hapana vyenginevyo wao ni katika mawalii wa shaytwaan. Yule ambaye anataka kuingia kwa kina zaidi jambo hili basi arejee katika kitabu “al-Furqaan” cha Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 251
  • Imechapishwa: 06/05/2025