33. Rak´ah mbili za Twawaaf wakati uliokatazwa

Swali 33: Ni ipi hukumu ya kuswali Rak´ah mbili nyuma ya mahali pa kusimama baba yetu Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika zile nyakati ambazo mtu amekatazwa kuswali swalah zilizopendekezwa[1]?

Jibu: Hapana neno kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Enyi wana wa ´Abdul-Manaaf! Msimzuie yeyote ambaye ametuku katika Nyumba hii na akaswali katika saa yoyote anayotaka ni mamoja usiku au mchana.”[2]

Ameipokea Imaam Ahmad na watunzi wa Sunan wanne kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

Isitoshe ni kwa sababu swalah ya Twawaaf ni miongoni mwa zile swalah zinazoswaliwa kutokana na sababu. Kwa hiyo hapana neno kuiswali katika wakati uliokatazwa kama mfano wa swalah ya mamkuzi ya msikiti, swalah ya kupatwa kwa jua kutokana na Hadiyth iliyotajwa na nyenginezo zilizopokelewa katika mlango huu. Mfano wa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika jua na mwezi ni alama mbili miongoni mwa alama za Allaah. Havipatwi kwa kufariki au kupata uhai kwa yeyote. Allaah kwavyo anawatia khofu waja Wake. Mkiona kitu katika hayo basi kimbilieni kumtaja, kumuomba, kumtaka msamaha, kutoa swadaqah, kuwaachia watumwa huru na kuswali misikitini mpaka iondoke hali hiyo.”[3]

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Anapoingia mmoja wenu msikitini, basi asiketi chini mpaka kwanza aswali Rak´ah mbili.”[4]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim katika “as-Swahiyh” zao kupitia kwa Abu Qataadah (Radhiya Allaahu ´anh).

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (11/291-292).

[2] Ahmad (16294),  at-Tirmidhiy (795) na an-Nasaa´iy (581).

[3] al-Bukhaariy (1000) na Muslim (1522).

[4] al-Bukhaariy (425) na Muslim (166).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 14/03/2022