2 – Amesema kuwa namna haitambuliki. Akili haziwezi kudiriki namna zilivyo sifa za Muumba (Subhaanah). Allaah (Ta´ala) ametamka hilo wazi:
وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا
“… na hawawezi kumzunguka kwa kumtambua.”[1]
Shaykh na ´Allaamah Muhammad al-Amiyn ash-Shanqiytwiy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Maana yake ni kwamba elimu ya mwanadamu haiwezi kumzunguka Mola wa mbingu na ardhi. Kwa hivyo maana hiyo inakanusha aina ya uzungukaji wa namna yake. Uzungukaji wa aina ya elimu ni yenye kukanushwa kwa Mola wa walimwengu. Kwa hiyo hupaswi kutatizika na kule kushuka, kuja, mkono, vidole, mshangao au kucheka kwa Allaah. Kwa sababu mtu anatakiwa kuchukua msimamo mmoja. Yale ambayo Allaah amejieleza kwayo ni haki na ni yenye kulingana na ukamilifu na utukufu Wake. Hakuna sifa yoyote ya viumbe inayofanana Naye. Yale ambayo viumbe wameelezwa kwayo pia ni haki na yanaendana na kushindwa kwao, kuteketea kwao na mahitaji yao. Maneno haya mengi Allaah ameyabainisha katika sentesi mbili:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[2]
Sentesi isemayo:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye… “
ni kutakasa pasi na kukansha.
وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“… Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”
ni kuamini bila ya kufananisha. Kwa hivyo Aayah nzima mosi inaamrisha utakasaji usiokuwa na ukanushaji, pili kuamini sifa Zake zote pasi na kufananisha. Kwa hiyo Aayah nzima inahusiana na imani. Yule anayeifanyia kazi utakaso unaopatikana katika jumla ya kwanza na akaamini jumla ya pili na akaacha kupekua namna, anakuwa mwenye kusalimika.”[3]
[1] 20:110
[2] 42:11
[3] Manhaj wa Diraasaat li Aayaat-il-Asmaa’ was-Swifaat, uk. 104-107.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 54-55
- Imechapishwa: 02/12/2025
2 – Amesema kuwa namna haitambuliki. Akili haziwezi kudiriki namna zilivyo sifa za Muumba (Subhaanah). Allaah (Ta´ala) ametamka hilo wazi:
وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا
“… na hawawezi kumzunguka kwa kumtambua.”[1]
Shaykh na ´Allaamah Muhammad al-Amiyn ash-Shanqiytwiy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Maana yake ni kwamba elimu ya mwanadamu haiwezi kumzunguka Mola wa mbingu na ardhi. Kwa hivyo maana hiyo inakanusha aina ya uzungukaji wa namna yake. Uzungukaji wa aina ya elimu ni yenye kukanushwa kwa Mola wa walimwengu. Kwa hiyo hupaswi kutatizika na kule kushuka, kuja, mkono, vidole, mshangao au kucheka kwa Allaah. Kwa sababu mtu anatakiwa kuchukua msimamo mmoja. Yale ambayo Allaah amejieleza kwayo ni haki na ni yenye kulingana na ukamilifu na utukufu Wake. Hakuna sifa yoyote ya viumbe inayofanana Naye. Yale ambayo viumbe wameelezwa kwayo pia ni haki na yanaendana na kushindwa kwao, kuteketea kwao na mahitaji yao. Maneno haya mengi Allaah ameyabainisha katika sentesi mbili:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[2]
Sentesi isemayo:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye… “
ni kutakasa pasi na kukansha.
وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“… Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”
ni kuamini bila ya kufananisha. Kwa hivyo Aayah nzima mosi inaamrisha utakasaji usiokuwa na ukanushaji, pili kuamini sifa Zake zote pasi na kufananisha. Kwa hiyo Aayah nzima inahusiana na imani. Yule anayeifanyia kazi utakaso unaopatikana katika jumla ya kwanza na akaamini jumla ya pili na akaacha kupekua namna, anakuwa mwenye kusalimika.”[3]
[1] 20:110
[2] 42:11
[3] Manhaj wa Diraasaat li Aayaat-il-Asmaa’ was-Swifaat, uk. 104-107.
Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 54-55
Imechapishwa: 02/12/2025
https://firqatunnajia.com/33-namna-ya-kulingana-juu-haitambuliki/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket