33. Je, anapewa udhuru anayemwomba asiyekuwa Allaah au kumuomba msaada asiyekuwa Allaah kutokana na ujinga wake?

Swali 33: Je, anayemwomba asiyekuwa Allaah au kumuomba msaada asiyekuwa Allaah kwa sababu ya ujinga wake anapewa udhuru?

Jibu: Tulishatangulia kuzungumzia mfano wa swali hili hapo kabla kwamba msingi ni kuwa mtu huyo hapewi udhuru ikiwa anaishi miongoni mwa waislamu na amefikiwa na ulinganizi. Lakini ikiwa atatizwa kwa sababu ya wanazuoni wa uovu au wanazuoni wa batili, basi shubuha yake inatakiwa kuondolewa na abainishiwe. Msingi wa jambo hilo ni kwa Ahl-ul-Fatrah. Ama baada ya kutumilizwa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa wale wanaoishi miongoni mwa waislamu, msingi ni kwamba hawapewi udhuru. marq Mara nyingi ni kwamba anayemwomba asiyekuwa Allaah au kumuomba msaada asiyekuwa Allaah hufanya hivyo kwa ukaidi na si kwa sababu ya kutojua jambo hilo.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 71
  • Imechapishwa: 09/01/2026