33. Hapo ndipo hufunguliwa milango ya mbingu

31 – Abu Umaamah amesimulia kwamba Ayyuub amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliikaa kwangu mwezi mmoja. Nikawa nachungana na matendo yake. Nikamuona pindi jua linapopinduka na huku mkononi mwake yuko na kitu cha kidunia, basi hukitupa. Na kama amelala, basi ni kama vile ameamshwa. Huamka, akaoga au akatawadha kisha akaswali Rak´ah nne, akizikamilisha, akazifanya uzuri na makini. Nikamuuliza juu ya hilo ambapo akasema: ”Hakika milango ya mbingu na milango ya Pepo hufunguliwa katika saa hiyo. Haifungwi mpaka tuiswali swalah hii. Hivyo hupenda kheri kutoka kwangu ipande kwa Mola wangu katika saa hiyo.”

Ameipokea Aadam bin Abiy Iyaas katika ”Kitaab-uth-Thawaab”. Cheni ya wapokezi wake ni dhaifu[1].

[1] Hata hivyo nukta ya mzozo katika Hadiyth inatiliwa nguvu na Hadiyth fupi ya ´Abdullaah bin as-Saaib:

“Milango ya mbingu hufunguliwa katika saa hiyo. Hivyo katika wakati huo hupenda yapande juu matendo yangu mema.”

Ameipokea at-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa ni nzuri, na Ahmad (03/411) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Ingelikuwa bora endapo mtunzi angeipa kipaumbele, kutokana na usahihi wa matini yake na ufupi wake.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 96
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy