Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifika Madiynah akawakuta mayahudi wanafunga siku ya ´Aashuuraa’. Walipoulizwa kuhusu hilo wakajibu kwamba hiyo ni siku ambayo Allaah alimnusuru Muusa na wana wa Israaiyl dhidi ya Fir’awn, basi kwa ajili hyio tunafunga kwa kuitukuza.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
“Sisi tuna haki zaidi kwa Muusa kuliko nyinyi.”
Kisha akaamrisha ifungwe.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Imekuja katika upokezi mwingine wa Muslim:
“Basi Muusa akaifunga kama shukrani, nasi tunafunga…”[1]
MAELEZO
Hadiyth hii inabainisha hekima kubwa ya kusuniwa kufunga siku ya ´Aashuuraa’, nayo ni kuitukuza siku hii na kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa kumuomoa Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wana wa Israaiyl na kuzamisha Fir’awn na watu wake. Kwa sababu hiyo Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaifunga kwa ajili ya kuonyesha shukrani kwa Allaah na mayahudi waliifunga pia. Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) una haki zaidi ya kumfuata Muusa kuliko mayahudi.
Kwa sababu hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
“Sisi ni aula zaidi kwa Muusa kuliko nyinyi.”
Imekuja katika upokezi mwingine:
“Mimi nina haki zaidi kwa Muusa kuliko nyinyi.”
Kwa maana ya kwamba sisi tuna ufuasi wa kweli na wa karibu zaidi kwa Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwani tunakubaliana naye katika msingi wa dini na tunasadikisha Kitabu Chake, ilihali nyinyi mnatofautiana naye kwa kugeuza na kupotosha.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mtii zaidi na mfuasi wa haki zaidi kuliko wao, kwa ajili hiyo akaifunga siku ya ´Aashuuraa’ na akaamrisha ifungwe, kwa ajili ya kuonyesha kuiheshimu siku hiyo na kuithibitisha nafasi yake.
Abu Muusa (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Siku ya ´Aashuuraa’ ilikuwa ni siku ambayo mayahudi wanaitukuza na kuifanya kama sikukuu. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
“Fungeni nyinyi.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Imekuja katika upokezi mwingine:
“Watu wa Khaybar walikuwa wakifunga siku ya ´Aashuuraa’ na kuifanya kama sikukuu na wanawake wao huvalishwa mapambo yao na mavazi yao ya sherehe.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
“Basi fungeni nyinyi.”[2]
Dhahiri ni kwamba miongoni mwa hekima ya kufunga siku hii ni kwenda kinyume na mayahudi kwa kutoifanya kuwa siku ya sikukuu, bali kuifunga tu, kwani siku ya ´Iyd haifungiwi, jambo ambalo ni la muhimu zaidi katika kwenda kinyume na mayahudi kuhusu ´Aashuuraa’. Na – Allaah akitaka – tutakuja kuona njia nyingine ya kwenda kinyume, nayo ni kufunga pia siku ya tisa kabla ya kumi.
[1] al-Bukhaariy (3943) na Muslim (1130), (127) na (128).
[2] al-Bukhaariy (2005) na Muslim (1131), (129) na (130).
- Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 60
- Imechapishwa: 20/05/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 60
Imechapishwa: 20/05/2025
https://firqatunnajia.com/33-hadiyth-sisi-tuna-haki-zaidi-kwa-muusa-kuliko-nyinyi/