144 – Abu Bakr Muhammad bin ´Umar bin al-Qaasim an-Narsiy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdullaah bin Ibraahiym ash-Shaafiy´iy ametuzindua: Haytham bin Mujaahid ametukhabarisha: Ishaaq bin adh-Dhwayf ametukhabarisha: Bishr bin al-Haarith amenambia:
”Hakika wewe umekuja sana kwenye vikao vyangu. Nataka kukuomba jambo. Wewe unazisoma Hadiyth na nachelea watu wasiuharibu moyo wangu. Kwa ajili hiyo nakuomba usirudi tena kwangu.”
Sikurudi tena kwake.
145 – Ibraahiym bin ´Umar al-Barmakiy ametukhabarisha: Abul-Fadhwl ´Ubaydullaah bin ´Abdir-Rahmaan az-Zuhriy ametukhabarisha: Hamzah bin al-Husayn bin ´Umar amenihadithia: Nimemsikia Ibraahiym bin Haani’ an-Naysaabuuriy akisema: Nimemsikia Bishr bin al-Haarith akisema:
”Nina nini mimi na Hadiyth? Nina nini mimi na Hadiyth? Hakika si vyenginevyo ni mtihani isipokuwa kwa yule ambaye amezitafuta kwa ajili ya Allaah.”
Amesimulia tena kwamba Bishr amesema:
”Wanasema kuwa mimi nakataza kuzisoma Hadiyth. Hata hivyo mimi sioni kama kuna kilicho bora kuliko yule mwenye kuzifanyia kazi. Kwa yule asiyezifanyia kazi bora kwake ni kuziacha.”
146 – al-´Atiyqiy ametukhabarisha: Muhammad bin al-´Abbaas ametuhadithia: Ja´far bin Muhammad as-Swandaliy ametuhadithia: Muhammad bin Yuusuf al-Jawhariy ametuzindua:
”Nilikuwa njiani kuelekea Baswrah na nikamwambia Bishr bin al-Haarith: ”Nimfikishie salamu Abul-Waliyd at-Twayaalisiy kutoka kwako?” Akasema: ”Hakika nyote wawili wewe na Abul-Waliyd mtakufa. Unataka uje kuulizwa kama ulisikia. Hakika umesikia. Kwa ajili hiyo yazingatie yale uliyoyasikia. Kwani usipoyafanyia kazi basi itakuwa ni majuto kwako siku ya Qiyaamah.”
147 – Abu Twaahir Muhammad bin al-Hasan bin Zayd bin al-Hasan al-´Alawiy ametukhabarisha huko Rayy: Ahmad bin Muhammad bin Sahl al-Bazzaaz ametuhadithia: Muhammad bin Ayyuub ametuhadithia: Siku moja Abul-Waliyd alisema maneno mfano wa:
”Hakuna wanachokusudia kwa Hadiyth hizi isipokuwa kukithirisha. Kichache kinatosha kwa yule anayemcha Allaah.” Kisha akasema maneno mfano wa: ”Wanazikusanya Hadiyth, wakazisimulia kwa cheni zilizoungana, na mengineyo kwa ajili ya kuzielekeza nyuso za watu kwake.”
148 – Abul-Mudhwaffar Hanaad bin Ibraahiym an-Nasafiy ametukhabarisha: Muhammad bin Ahmad bin Muhammad bin Sulaymaan al-Haafidhw ametukhabarisha huko Bukhaaraa: Nimemsikia Abu Swaalih Khalaf bin Muhammad akisema: Nimemsikia Abu Bakr bin ´Abdillaah bin Ja´far – yaani at-Taajir – akisema:
”Nimemsikia Ahmad bin Hanbal akiulizwa juu ya mtu ambaye anaziandika Hadiyth kwa wingi. Akasema: ”Kila ambavyo anazidisha kuzitafuta Hadiyth ndivo anavyotakiwa kuzidi kuzifanyia kazi.” Kisha akasema: ”Kwani pesa ni kama mali; kila ambavyo mali inazidi, ndivo inavyozidi zakaah yake.”
149 – Muhammad bin al-Husayn bin al-Fadhwl al-Qattwaan ametukhabarisha: Da´laj bin Ahmad ametukhabarisha: Ahmad bin ´Aliy al-Aabaar ametuzindua: Abu ´Ammaar al-Husayn bin Hurayth ametuhadithia: Wakiy´ bin al-Jarraah ametuhadithia, kutoka kwa Ibraahiym bin Ismaa´iyl bin Mujammy´, ambaye amesema:
”Kilichokuwa kinatusaidia kuzihifadhi Hadiyth ni kuzifanyia kazi.”
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 86-88
- Imechapishwa: 22/05/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)