173 – al-Huutiy ametukhabarisha: Baqiyyah ametukhabarisha: Buhayr bin Sa´iyd ametukhabarisha, kutoka kwa Khaalid bin Ma´daan, kutoka kwa Jubayr bin Nufayr, kutoka kwa ´Awf bin Maalik, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtamiminiwa dunia kiasi cha kwamba hakuna kitachokupindisheni baada yangu isipokuwa yenyewe.”[1]
174 – Hishaam bin ´Ammaar ametukhabarisha: Muhammad bin ´Iysaa ametukhabarisha, kutoka kwa Ibraahiym bin Sulaymaan, kutoka kwa al-Waliyd bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Jubayr bin Nufayr, kutoka kwa Abud-Dardaa’, ambaye amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtamiminiwa dunia kiasi cha kwamba moyo wa mmoja wenu ikiwa utapinda basi hautopinda isipokuwa kwa yenyewe.”[2]
175 – Abu Bakr ametukhabarisha: Muhammad bin Fudhwayl ametukhabarisha, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Ziyaad, kutoka kwa Zayd bin Wahb, kutoka kwa Abu Dharr, ambaye amesema:
“Mtu mmoja alisimama na kusema: “Ee Mtume wa Allaah, fisi inatula!” Ndipo akasema: “Ninachofia zaidi kwenu ni ni kwamba hakika mtamiminiwa dunia.”[3]
Nikasema kumwambia Yaziyd: “Nini maana ya fisi?” Akasema: “Ukame.”
176 – Ibn Musaffaa ametuhadithia: Yahyaa bin Sa´iyd ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdir-Rahmaan ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdullaah bin Busr, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Naapa kwa yule Ambaye nafsi yangu imo mkononi Mwake! Mtazifungua nchi za Waajemi na dunia itakuja kumiminwa kwenu.”
[1] Ahmad (23462). Swahiyh kupitia zingine kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (3257).
[2] Ibn Maajah (5). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (9).
[3] Ahmad (20846). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (1894).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 43-44
- Imechapishwa: 08/07/2025

Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 43-44
Imechapishwa: 08/07/2025
https://firqatunnajia.com/32-ulimwengu-kumiminwa-juu-yetu/