16 – Kubadilishana ujumbe wa kimapenzi

Miongoni mwa makosa yanayopingana na Shari´ah ni kubadilishana jumbe za kimapenzi kati ya baadhi ya wasichana. Kuna aina fulani ya jambo hili ambayo hujulikana kama “telegrafu”. Khatari zaidi ni pale linapofanyika kati ya vijana wa kiume na wa kike. Hivyo basi mche Allaah, ee mja wa Allaah, katika yale unayosema na kuandika. Andika nasaha zenye manufaa katika telegrafu ili upate faida na kuwafaidisha wengine.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 11/03/2026