Ahl-ul-Bid´ah wanafanya tofauti na mfumo huu. Wamegawanyika mafungu yafuatayo:

1 – Mumaththilah waliothibitisha na kufananisha.

2 – Mu´attwilah waliokanusha na kupinga.

Ahl-us-Sunnah ni wenye kujitenga na mapote yote mawili. Mumaththilah ni makafiri. Mu´attwilah pia ni makafiri. Ama kuhusu Ahl-us-Sunnah wao ndio ambao wamethibitisha pasi na kufananisha, kwa maana wamethibitisha sifa na majina Yake kwa njia inayolingana na Allaah. Ni uthibitishaji usiokuwa na ufananishaji. Sambamba na hilo wakamtakasa kushabihiana na viumbe Vyake, utakaso usiokuwa ndani yake na ukanushaji. Tofauti na wanavyofanya Mumaththilah na tofauti vilevile na Mu´attwilah katika Jahmiyyah, Mu´tazilah na vijukuu vyao.

Inatakikana, bali ni wajibu kwa muumini kufuata mfumo huu wa Ahl-us-Sunnah ambao ni Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wenye kuwafuata kwa wema. Ukiulizwa ni kina nani Ahl-us-Sunnah? Jibu sema kuwa ni Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na waliowafuata kwa wema ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa Maswahabah, wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah, maimamu wanne na Ahl-us-Sunnah wengineo. Hawa ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Mwenye kwenda kinyume nao si katika wao. Mwenye kuthibitisha kupindukia, akafananisha au akakanusha [sifa za Allaah] basi ni katika Ahl-ul-Bid´ah. Ahl-us-Sunnah wamejitenga mbali kutokana na wao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 44
  • Imechapishwa: 22/10/2024