30 – ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kizazi kimening´inizwa na ´Arshi. Na si yule mwenye kuunga ndiye anayekihifadhi, lakini ambaye anakihifadhi ni ambaye anapokatwa na jamaa yake basi yeye anamuunga.”[1]

Cheni ya wapokezi wake ni yenye nguvu.

[1] Ahmad (2/163) na (2/193). Cheni ya wapokezi wake ni swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy. al-Bukhaariy ameipokea katika “as-Swahiyh” yake pasi na ”Kizazi kimening´inizwa na ´Arshi”. Imesahihishwa na at-Tirmidhiy. Ziada hii inatiliwa nguvu na Hadiyth nyingi kutoka kwa jopo la Maswahabah, ikiwa ni pamoja na ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwa al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 95-96
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy