122-
لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ الْعَظـيمُ الْحَلِـيمْ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ رَبُّ العَـرْشِ العَظِيـمِ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ رَبُّ السَّمَـوّاتِ ورّبُّ الأَرْضِ ورَبُّ العَرْشِ الكَـريم
”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, Aliye mtukufu, Mwenye kuvumilia, Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, Mola wa ‘Arshi tukufu, Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, Mola wa mbingu, Mola wa ardhi na Mola wa ‘Arshi tukufu.”[1]
123-
اللّهُـمَّ رَحْمَتَـكَ أَرْجـو فَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـيْن، وَأَصْلِـحْ لي شَأْنـي كُلَّـه لَا إِلَهَ إِلَّا أنْـت
“Ee Allaah! Rehma Zako nataraji, usinitegemeze katika nafsi yangu japo kwa muda wa kupepesa jicho na unitengenezee mambo yangu yote; hapana mungu wa haki mwengine isipokuwa Wewe.”[2]
124-
لاَ إِلَهَ إِلَّا أنْـت سُـبْحانَكَ إِنِّي كُنْـتُ مِنَ الظّـالِميـن
”Hapana mungu wa haki mwengine isipokuwa Wewe; kutakasika kutokamana na mapungufu ni Kwako, hakika mimi ni miongoni mwa waliojidhulumu.”[3]
125-
اللهُ اللهُ رَبِّي لا أُشْـرِكُ بِهِ شَيْـئاً
“Allaah, Allaah ndiye Mola wangu; simshirikishi Yeye na chochote.”[4]
[1] al-Bukhaariy (07/154) na Muslim (04/2092).
[2] Abu Daawud (04/324) na Ahmad (05/42). Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Abiy Daawuud” (03/959).
[3] at-Tirmidhiy (05/529) na al-Haakim ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye (01/505). Tazama ”Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/168).
[4] Abu Daawuud (02/87). Tazama ”Swahiyh Ibn Maajah” (02/335).
- Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huswn-ul-Muslim
- Imechapishwa: 29/04/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)