Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

52 – Yule atakayehoji kuhusu matendo Yake basi amerudisha hukumu ya Kitabu, na yeyote anayerudisha nyuma hukumu ya Kitabu anakuwa miongoni mwa makafiri. Haya ni baadhi ya yale ambayo anayahitaji yule ambaye moyo wake umetiwa nuru miongoni mwa wale mawalii wa Allaah (Ta´ala) na ni ngazi ya wale ambao wamebobea katika elimu. Kwa sababu kuna sampuli mbili za elimu: elimu inayopatikana kwa viumbe na elimu iliyokosekana kwa viumbe. Kupinga elimu iliopo ni ukafiri na kudai elimu isiyopatikana ni ukafiri. Haithibiti imani isipokuwa kwa kukubali elimu iliopo na kuacha kutafuta elimu isiyopatikana.

MAELEZO

Ibn Abiyl-´Izz al-Hanafiy amesema:

”Anaashiria yale yaliyokwishatangulia na ambayo ni lazima kuyaamini na kuyatendea kazi ambayo yamekuja na Shari´ah. Kusema kwamba ni ngazi ya wale waliobobea katika elimu kunamaanishwa ulimi ya yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) elimu ya jumla na iliyopambanuliwa, elimu ya mambo yaliyokanushwa na mambo yaliyothibitishwa. Elimu iliyokosekana kunakusudiwa elimu ya makadirio ambayo Allaah ameificha kwa watu na akawazuia kutokana na kuifuatilia. Elimu inayopatikana kunakusudiwa elimu ya Shari´ah kuanzia misingi mpaka tanzu zake. Yule mwenye kupinga chochote katika yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi anakuwa miongoni mwa makafiri. Na yule mwenye kudai kujua elimu iliyofichikana pia anakuwa ni miongoni mwa makafiri.”[1]

[1] Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (1/343).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 45-46
  • Imechapishwa: 25/09/2024