´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema katika ugonjwa wake: “Mwamrishe Abu Bakr awaswalishe watu.” Nikasema: ”Abu Bakr akisimama mahali pako basi watu hawatosikia kutokana na kilio chake. Hebu mwache ´Umar aswalishwe.” Akasema: “Mwamrishe Abu Bakr awaswalishe watu.” ´Aaishah akamwambia Hafswah: “Mwambie: ”Abu Bakr akisimama mahali pako basi watu hawatosikia kutokana na kilio chake. Hebu mwache ´Umar awaswalishe watu.” Hafswah akafanya hivo ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Hakika nyinyi ni kama wakeze Yuusuf. Mwamrishe Abu Bakr awaswalishe watu.” Hafswah akamwambia ´Aaishah: “Sikupata faida yoyote kutoka kwako.”[1]

[1] al-Bukhaariy (716) na Muslim (418).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 23/06/2025