Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
15 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akibusu hali ya kuwa amefunga na akichanganyikana ilihali amefunga, lakini alikuwa ni mwenye kuweza kujizuia vyema kuliko nyinyi.”[1]
Hadiyth ni dalili kwamba inajuzu kwa mwenye kufunga kumbusu mke wake na kumgusa kwa mwili na kwamba jambo hilo haliharibu swawm wala kupunguza thawabu zake.
Makusudio ya ”kuchanganyikana” ni kugusana ngozi mbili kwa mwili au kwa namna nyingine kama hiyo. Ni neno pana zaidi kuliko kubusu. Mara nyingine linaweza kutumika kumaanisha tendo la ndoa, lakini hapa haimaanishi hivyo. at-Twahaawiy amepokea kwa cheni yake kupitia kwa Hakiym bin ‘Iqaal ambaye amesema:
”Nilimuuliza ‘Aaishah kuhusu ni kipi kilichoharamishwa kwangu kutoka kwa mke wangu nikiwa nimefunga?” Akasema: ”Uke wake.”[2]
´Abd-ur-Razzaaq amepokea kwa cheni yake kupitia kwa Masruuq ambaye amesema:
”Nilimuuliza ‘Aaishah kuhusu ni kipi kilichoharamishwa kwa mwanaume kutoka kwa mke wake akiwa amefunga?” Akasema: ”Kila kitu isipokuwa tendo la ndoa.”[3]
[1] al-Bukhaariy (1927) na Muslim (1106).
[2] Sharh Ma´aaniy-il-Aathaar (2/95). Amesema katika “Fath-ul-Baariy” (4/149): ”Cheni ya wapokezi mpaka kwa al-Haakim ni Swahiyh.”
[3] al-Muswannaf (04/190). Amesema katika “Fath-ul-Baariy” (4/149): ”Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.”
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/40-41)
- Imechapishwa: 12/02/2025
Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
15 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akibusu hali ya kuwa amefunga na akichanganyikana ilihali amefunga, lakini alikuwa ni mwenye kuweza kujizuia vyema kuliko nyinyi.”[1]
Hadiyth ni dalili kwamba inajuzu kwa mwenye kufunga kumbusu mke wake na kumgusa kwa mwili na kwamba jambo hilo haliharibu swawm wala kupunguza thawabu zake.
Makusudio ya ”kuchanganyikana” ni kugusana ngozi mbili kwa mwili au kwa namna nyingine kama hiyo. Ni neno pana zaidi kuliko kubusu. Mara nyingine linaweza kutumika kumaanisha tendo la ndoa, lakini hapa haimaanishi hivyo. at-Twahaawiy amepokea kwa cheni yake kupitia kwa Hakiym bin ‘Iqaal ambaye amesema:
”Nilimuuliza ‘Aaishah kuhusu ni kipi kilichoharamishwa kwangu kutoka kwa mke wangu nikiwa nimefunga?” Akasema: ”Uke wake.”[2]
´Abd-ur-Razzaaq amepokea kwa cheni yake kupitia kwa Masruuq ambaye amesema:
”Nilimuuliza ‘Aaishah kuhusu ni kipi kilichoharamishwa kwa mwanaume kutoka kwa mke wake akiwa amefunga?” Akasema: ”Kila kitu isipokuwa tendo la ndoa.”[3]
[1] al-Bukhaariy (1927) na Muslim (1106).
[2] Sharh Ma´aaniy-il-Aathaar (2/95). Amesema katika “Fath-ul-Baariy” (4/149): ”Cheni ya wapokezi mpaka kwa al-Haakim ni Swahiyh.”
[3] al-Muswannaf (04/190). Amesema katika “Fath-ul-Baariy” (4/149): ”Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.”
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/40-41)
Imechapishwa: 12/02/2025
https://firqatunnajia.com/31-hadiyth-mtume-wa-allaah-alikuwa-akibusu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket