29- Abul-Qaasim Yahyaa bin Ahmad bin ´Aliy as-Siybiy al-Qisriy ametukhabarisha: Abu ´Aliy al-Hasan bin Ahmad bin Ibraahiym bin Shaadhaan ametuhadithia: Abu Bakr Ahmad bin Kaamil bin Khalaf ametuhadithia: Muhammad bin Sa´d al-´Awfiy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Bakr as-Sahmiy ametuhadithia: Yaziyd bin ´Awaanah ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Dhakwaan, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar ambaye amesema:
“Siku moja tulikuwa tumekaa mzunguko kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na tahamaki akapita mmoja katika wasichana zake. Mtu mmoja akasema: “Huyu ni msichana wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” Abu Sufyaan akasema: “Muhammad ukilinganisha na Banuu Haashim ni kamam mfano wa nyasi zilizo kati ya ndovu.”Mwanamke yule akayasikia maneno hayo na akamfikishia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatoka, nadhani kuwa alikuwa na hasira, akapanda juu ya mimbari na kusema: “Wana nini watu fulani ambao wanazungumza kwa njia hiyo? Allaah ameumba mbingu saba, akachagua kuishi katika ile iliyo juu zaidi na akawafanya viumbe Wake wengine awatakao kuishi katika mbingu zeengine. Halafu akaumba ardhi saba, akachagua iliyo juu zaidi na akawafanya wale viumbe awatakao kuishi juu yake. Kisha akachagua katika viumbe Wake na akawachagua wanaadamu, kutoka katika wanaadamu akawachagua waarabu, kutoka katika waarabu akawachagua Mudhar, kutoka Mudhara akawachagua Quraysh, kutoka Quraysh akawachagua Banuu Haashim, kutoka Banuu Haashim akawachagua akanichagua mimi. Mimi ndiye mbora wa wabora. Nampenda yule anayewapenda Quraysh na namchukia yule anayewachukia waarabu.”[1]
[1] al-Albaaniy amesema::
”Dhaifu sana.” (Silsilat-ul-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah (1/345))
- Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 117-118
- Imechapishwa: 10/06/2018

Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 117-118
Imechapishwa: 10/06/2018
https://firqatunnajia.com/31-dalili-ya-ishirini-na-tisa-kutoka-katika-sunnah-kwamba-allaah-yuko-juu-ya-viumbe/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)