31. Allaah alikuwa juu ya ´Arshi Yake kabla ya kuumba chochote

29 – Mujaahid amesema:

”Ibn ´Abbaas aliambiwa kwamba kuna watu wanaopinga Qadar. Akasema: ”Wanakadhibisha Uandishi. Nikishika unywele wa mmoja wao, basi ningeliung´oa. Allaah (´Azza wa Jall) alikuwa juu ya ´Arshi Yake kabla ya kuumba chochote. Akaumba viumbe na akaandika yale yatayokuwepo mpaka siku ya Qiyaamah. Watu wanapita katika mambo ambayo tayari yamekwishaamuliwa.”[1]

[1] Mtunzi katika asili ametaja cheni ya wapokezi wake ambayo ni Swahiyh. Imepokelewa vilevile na al-Aajurriy katika “ash-Shariy´ah”, uk. 293, al-Laalakaa’iy katika “Sharh I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah”, uk. (1/91/2) na Ibn Qudaamah katika “Ithbaat Swifat-il-´Uluww” (62).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 95
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy