Swali 30: Ni ipi hukumu ya kuwafanyia mapenzi makafiri na washirikina? Na ni lini mapenzi haya yanakuwa ni ukafiri mkubwa unaomtoa mtu katika dini na ni lini yanakuwa ni dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa?
Jibu: Kuwafanyia mapenzi makafiri na washirikina, ikiwa ni kwa kuwapenda kwa moyo, ni ukafiri na ni kuritadi; kwa namna ya mtu akawapenda kwa moyo na hilo likasababisha kuwanusuru na kuwasaidia kwa mali, silaha au kwa maoni. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ
“Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na manaswara marafiki – wao kwa wao ni marafiki – na yeyote atakayewafanya marafiki basi yeye ni katika wao. Hakika Allaah haongoi watu madhalimu.”[1]
لَّا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّـهِ فِي شَيْءٍ إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً
”Waumini wasiwafanye makafiri kuwa marafiki wandani na walinzi badala ya Waumini. Na atakayefanya hivyo, basi hatokua na chochote mbele ya Allaah, isipokuwa ikiwa kwa ajili ya kujilinda hatari kutoka kwao. Na Allaah Anakutahadharisheni na Nafsi Yake. Na kwa Allaah ni mahali pa kuishia.”[2]
لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ
“Hutopata watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake, japo wakiwa ni baba zao, watoto wao, ndugu zao au jamaa zao… ”[3]
Kwa hivyo kuwapenda makafiri ni ukafiri na kuritadi, kwa sababu msingi wa mapenzi ni mapenzi ya moyoni halafu hilo linapelekea katika nusura na usaidizi. Ama Muwaalaah ni dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa; kwa namna ya kwamba mtu akaishi na kafiri, kuwa na urafiki naye, kujikomba kwake, kumsaidia kafiri nayepiga vita Uislamu hata kwa jambo dogo kama vile kumpa kalamu au kitu kingine. Kwa sababu hiyo wanazuoni wametaja kuwa hata kumsaidia kwa kumpa kitu kama hicho ni katika Muwaalaah na ni miongoni mwa madhambi makubwa. Lakini kafiri wa ahadi ambaye kuna mkataba baina yake na waislamu, hapana vibaya kumfanyia wema. Lakini kafiri anayepiga vita Uislamu haifai kabisa kumsaidia kwa aina yoyote ya msaada.
Kwa kumalizia ni kwamba mapenzi ya ndani yenye kupelekea msaada na nusura ni ukafiri na kuritadi. Lakini Muwaalaah, mchangamano na maingiliano yasiyozidi mipaka yaliyoamuliwa na watawala, kutokana na haja, ni dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa.
[1] 05:51
[2] 03:28
[3] 58:22
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 66-67
- Imechapishwa: 09/01/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 66-67
Imechapishwa: 09/01/2026
https://firqatunnajia.com/30-ni-lini-mapenzi-na-urafiki-na-makafiri-inakuwa-kufuru-kubwa-na-ni-lini-inakuwa-dhambi-kubwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket