14 – Kuvaa mavazi ya kubana na mafupi

Miongoni mwa makosa yanayoenda kinyume na Shari´ah ni kuvaa mavazi yenye kubana na mafupi, jambo ambalo huzungatiwa ni katika kuonyesha mapambo na uso. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kuna watu aina mbili wa Motoni sijawaona” akataja mmoja katika wao ”… na wanawake waliovaa vibaya, uchi.”[1]

Mwanamke ambaye amevaa nguo za kubana na fupi anaonekana kuwa amevaa, lakini kiukweli ni kwamba yuko uchi. Kwa sababu mavazi ya kubana yanauchora mwili na kuonyesha mapambo yake. Kwa hivyo jihadhari na mavazi ya kubana na mafupi.

[1] Muslim na Ahmad.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 30
  • Imechapishwa: 03/03/2026