30. Matahadharisho ya kusoma kwa lengo la umaarufu na kutafuta wafuasi

125 – al-Qaadhwiy Abu Bakr Ahmad bin al-Hasan bin Ahmad al-Hiyriy ametukhabarisha huko Naysaabuur: Abu Muhammad Haajib bin Ahmad bin Yarham bin Sufyaan at-Twusiy ametukhabarisha: Muhammad bin Hammaad – yaani al-Abiyawardiy – ametukhabarisha: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia, kutoka kwa Sulaymaan at-Tamiymiy, kutoka kwa Sayyaar, kutoka kwa ´Aa-idhullaah, ambaye amesema:

”Anayezifuatilia Hadiyth kwa ajili ya kuzisimulia, basi hatonusa harufu ya Pepo.”

126 – Abul-Hasan ´Aliy bin al-Qaasim bin al-Hasan ash-Shaahid ametukhabarisha huko Baswrah: ´Aliy bin Ishaaq al-Maadiraa-iy ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad al-Khaliyliy ametukhabarisha: Sulaymaan bin Daawuud amenihadithia: Khaalid bin al-Haarith al-Hujaymiy ametukhabarisha: Kulisemwa kuambiwa Ibn Shubrumah:

”Simulia utalipwa thawabu.” Ndipo akasoma:

Wananiahidi malipo makubwa illihali hakuna ninachotamani

isipokuwa kuokoka – isiwe upande wangu wala dhidi yangu

127 – al-Qaadhwiy Abul-´Alaa’ al-Waasitwiy ametukhabarisha: Muhammad bin Ahmad bin Muhammad al-Mu´iyd ametuzindua kwa njia ya kutusomea: Muhammad bin as-Simtw ametuhadithia: Abu Naswr Rajaa’ bin Sahl ametukhabarisha: Abu Mushir ´Abdul-A´laa bin Mushir ametuhadithia:

”Asubuhi moja wanafunzi waliraukia kwa al-Awzaa´iy kwa ajili ya kusikiliza Hadiyth, ambapo akawageukia na kusema:

Ni wakusanyaji wangapi wenye pupa na wenye hamu

Wasiokuwa wenye kunufaika wala kunufaisha!

128 – ´Aliy bin al-Qaasim ametukhabarisha: ´Aliy bin Ishaaq ametukhabarisha: al-Mufadhdhwal bin Muhammad bin Ibraahiym alisomewa huko Makkah na mimi nimehudhuria: Abu Ya´quub Ishaaq bin Ibraahiym at-Twabariy ametukhabarisha: Nimemsikia al-Fudhwayl akisema:

”Lau ungeniomba dinari ingelikuwa ni jambo jepesi zaidi kwangu kuliko kuniomba kusimulia Hadiyth.” Nikamwambia: ”Kunisimulia faida ya Hadiyth ambazo nilikuwa sina inapendeza zaidi kwangu kuliko kunipa dinari.” Akasema: ”Hakika wewe umetahiniwa. Naapa kwa Allaah kuyafanyia kazi yale ambayo umekwishasikia kungekushughulisha kutokana na yale ambayo hujayasikia.” Kisha akasema: ”Nimemsikia Sulaymaan bin Mihran akisema: ”Ni lini utashiba ikiwa kila unapochukua tonge la chakula mdomoni unalitupa nyuma ya mgongo wako?”

129 – ´Aliy bin al-Qaasim ametukhabarisha: ´Aliy bin Ishaaq al-Maadiraa-iy ametukhabarisha: Ja´far bin Muhammad as-Swaa-igh ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin ´Umar al-Qazwiyniy ametukhabarisha:

”Nilimuona mtoto wa Sufyaan bin ´Uyaynah amekuja kwa al-Fudhwayl, akamwambia: ”Je, hayakutoshi yale yaliyoko katika nyumba yenu mpaka uhitaji kuja hapa?”

Bi maana Hadiyth.

130 – ´Aliy ametukhabarisha: ´Aliy ametuhadithia: Ja´far as-Swaa-igh ametukhabarisha: Khaalid bin Khidaash ametukhabarisha:

”al-Fudhwayl alinambia: ”Sufyaan amekuja?” Nikasema: ”Ndio.” Akasema: ”Alikuwa mtu mwema kabisa kama tu asingekuwa anazitafuta Hadiyth.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 81-83
  • Imechapishwa: 21/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy