Tunaweza kufupisha yote tuliyoyataja kwa vipengele sita vilivyotajwa na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ambavyo ametaja dalili za wazi kabisa ya kwamba maana ni yenye kutambulika na inatakiwa kutambuliwa:
“Cha kwanza kinapelekea kwamba, kutokana na desturi ya kimaumbile ambayo Allaah amewaumba kwayo wanadamu, inapelekea kuitilia umuhimu Qur-aan ambayo wameteremshiwa, inapokuja katika matamshi na maana. Bali kwamba wanatakiwa kutilia bidii zaidi maana. Ni jambo linalotambulika ya kwamb mwenye kusoma kitabu kinachohusiana na tiba, hisabati, sarufi au Fiqh lazima kwa kiasi fulani awe na shauku ya kutaka kukifahamu na kuelewa maana yake. Basi kusemwe nini juu ya wale wanaosoma Kitabu cha Allaah (Ta’ala) walichoteremshiwa na akawaongoza kwacho na kwacho akawafundisha kupambanua baina ya haki na batili, kilicho chema na kibaya, uongofu na upotofu, ya sawa na ya makosa? Ni jambo linalotambulika ya kwamba ile hamu yao ya kutaka kukifahamu na kuelewa maana yake itakuwa ni miongoni mwa matakwa yao makubwa kabisa. Bali inatosha kwa mwanafunzi pale anaposikia maneno fulani kutoka kwa mwalimu wake anakuwa na shauku ya kutaka kuyafahamu. Basi kusemwe nini kwa yule anayesikia maneno ya Allaah yanayofikishwa kutoka Kwake? Bali ni jambo linalotambulika ya kwamba hamu yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ya kuwafahamisha maana ya Qur-aan ilikuwa makubwa zaidi kuliko hamu yake ya kuwafunza herufi zake. Utambuzi wa herufi pasi na maana hakufikiwi malengo yoyote. Kwani makusudio ya matamshi ni ile maana.
Pili ni kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) mara nyingi amewahimiza kuizingatia, kuielewa na kuifuata. Amesema (Ta’ala):
كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُوْلُوا الْأَلْبَابِ
“Kitabu Tumekiteremsha kwako chenye baraka ili wapate kuzingatia kwa makini Aayah zake na ili wapate kukumbuka wale wenye akili.”[1]
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ أَمْ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقْفَالُهَا
“Je, hawaizingatii Qur-aan au nyoyoni mwao mna kufuli?”[2]
أَفَلَمْ يَدَّبَّرُوا الْقَوْلَ
”Je, hawakuzingatia kauli?”[3]
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ ۚ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ اللَّـهِ لَوَجَدُوا فِيهِ اخْتِلَافًا كَثِيرًا
“Je hawaizingatii Qur-aan? Na lau ingelikuwa imetoka kwa asiyekuwa Allaah, bila shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi.”[4]
Ikiwa amewahimiza makafiri na wanafiki kuizingatia, basi mtu anapata kutambua kwamba maana yake makafiri na wanafiki wote wanaweza kuifahamu na kuijua. Ni vipi basi hilo lisiwezekane juu ya waumini? Hilo linathibitisha kwamba maana zake zilikuwa zenye kutambulika na zenye kuwabainikia.”
[1] 38:29
[2] 47:24
[3] 23:68
[4] 4:82
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 50-51
- Imechapishwa: 01/12/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 50-51
Imechapishwa: 01/12/2025
https://firqatunnajia.com/30-kila-mtu-anaweza-kuifahamu-qur-aan/