Allaah (Ta´ala) amesema:
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنَّكَ تَرَى الْأَرْضَ خَاشِعَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ
”Miongoni mwa alama Zake ni kwamba utaona ardhi imetulia kame, kisha tunapoiteremshia maji inataharaki na kuotesha.”[1]
Kutetemeka na kuinuka kwake ni kupanda kwake, jambo ambalo linaondosha kule kunyenyekea kwake. Kwa hivyo ikafahamisha kwamba unyenyekevu wake upo katika kutulia na kunyenyekea kwake. Vilevile ndivo inavyokuwa kwa moyo. Inaponyenyekea, basi yanaondoka mawazo yake na matakwa yake mabaya, ambayo yanatokana na kule kufuata matamanio, matokeo yake unamnyenyekea Allaah. Hivyo kunaondoka kile kiburi, kujikweza na majivuno yaliyomo ndani yake. Wakati mambo hayo yanapokuwa moyoni, basi viungo vya mwili na matikisiko mpaka sauti inanyenyekea. Allaah (Ta´ala) amezieleza sauti kwa kunyenyekea pale aliposema:
وَخَشَعَتِ الْأَصْوَاتُ لِلرَّحْمَـٰنِ
“… sauti zitamnyenyekea Mwingi wa rehema… ”[2]
Unyenyekevu wa sauti upo katika ukimya baada ya mazungumzo. Vivyo hivyo ndivo Alivyoeleza nyuso na macho ya makafiri siku ya Qiyaamah kwa unyenyekevu, jambo ambalo limefahamisha unyenyekevu unaviathiri viungo vyote hivi vya mwili.
[1] 41:39
[2] 20:108
- Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 35-36
- Imechapishwa: 24/11/2025
Allaah (Ta´ala) amesema:
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنَّكَ تَرَى الْأَرْضَ خَاشِعَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ
”Miongoni mwa alama Zake ni kwamba utaona ardhi imetulia kame, kisha tunapoiteremshia maji inataharaki na kuotesha.”[1]
Kutetemeka na kuinuka kwake ni kupanda kwake, jambo ambalo linaondosha kule kunyenyekea kwake. Kwa hivyo ikafahamisha kwamba unyenyekevu wake upo katika kutulia na kunyenyekea kwake. Vilevile ndivo inavyokuwa kwa moyo. Inaponyenyekea, basi yanaondoka mawazo yake na matakwa yake mabaya, ambayo yanatokana na kule kufuata matamanio, matokeo yake unamnyenyekea Allaah. Hivyo kunaondoka kile kiburi, kujikweza na majivuno yaliyomo ndani yake. Wakati mambo hayo yanapokuwa moyoni, basi viungo vya mwili na matikisiko mpaka sauti inanyenyekea. Allaah (Ta´ala) amezieleza sauti kwa kunyenyekea pale aliposema:
وَخَشَعَتِ الْأَصْوَاتُ لِلرَّحْمَـٰنِ
“… sauti zitamnyenyekea Mwingi wa rehema… ”[2]
Unyenyekevu wa sauti upo katika ukimya baada ya mazungumzo. Vivyo hivyo ndivo Alivyoeleza nyuso na macho ya makafiri siku ya Qiyaamah kwa unyenyekevu, jambo ambalo limefahamisha unyenyekevu unaviathiri viungo vyote hivi vya mwili.
[1] 41:39
[2] 20:108
Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 35-36
Imechapishwa: 24/11/2025
https://firqatunnajia.com/3-unyenyekevu-unaathiri-viungo-vyote-vya-mwili/