3. Ndoa katika Uislamu inahitajia mapenzi

Ndoa katika dini yetu inahausiani na mkataba wa kihisia kati ya watu wawili. Wakati Muislamu anapooa anajua kuwa ndoa inahitajia mapenzi, amani, utulivu na furaha kwa wanandoa wote wawili. Mola Wetu (Subhaanahu wa Ta´ala) Amesema:

وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

“Na katika alama Zake ni kwamba Amekuumbieni kutokana na nafsi zenu [jinsi moja] wake ili mpate utulivu kwao; na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na Rahmah. Hakika katika
hayo bila shaka [kuna] alama kwa watu wanaotafakari.”[1]

Lau watu wangelishikamana na ujumbe wa Uislamu kuhusiana na suala la ndoa bila ya shaka yoyote wangelipendana na nyumba na mazingira yao yangelijaa mapenzi. Kutokamana na yaliyotajwa Uislamu umempa mume na mke haki zenye kuwapa maisha yenye kufurahikia, yenye utulivu, yenye furaha na maisha imara yaliyo na mapenzi, ukweli na utakaso.

[1] 30:21

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 9
  • Imechapishwa: 23/03/2017