Miongoni mwa misingi hiyo ni:
“… kuepuka Bid´ah…”
Kujiepusha na Bid´ah. Bid´ah maana yake ni maangamivu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa makundi yote yaliyotumbukia katika Bid´ah yataingia Motoni. Hili ni kwa sababu yanafuata vijia vya mashaytwaan:
وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ
“Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka – hivyo basi ifuateni na wala msifuate njia za vichochoro zikakufarikisheni na njia Yake.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipiga msitari wa kunyooka chini na kusema:
“Hii ni njia ya Allaah.”
Halafu akapiga msitari kushotoni na kuliani mwake na kusema:
“Hivi ni vijia. Katika kila njia kuna shaytwaan anayelingania kwayo.”[2]
Mwenye kuacha njia iliyonyooka katika ´Aqiydah, ´ibaadah, uelewa au mfano wa hayo amechukua njia ambayo shaytwaan analingania kwayo. Tahadharini sana na Bid´ah na upotevu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule mwenye kuzua katika amri yetu hii yasiyokuwemo, basi atarudishiwa mwenyewe.”[3]
Isitoshe Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametahadharisha juu ya Ahl-ul-Bid´ah na akasoma Kauli ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala):
هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ
“Yeye ddiye Aliyeteremsha kwako Kitabu – humo mna Aayah zilizo na maana ya wazi – hizo ndio msingi wa Kitabu – na nyinginezo zisizokuwa wazi maana. Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotevu hufuata zile zisizokuwa wazi maana zake kutafuta fitina na kutafuta kuzipindisha, na hakuna ajuae maana zake isipokuwa Allaah. Ama wale waliobobea katika elimu husema: “Tumeziamini; zote ni kutoka kwa Mola wetu”, na hawakumbuki isipokuwa wale wenye akili.”[4]
Aliposoma Aayah hii (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
“Mkiwaona wale wenye kufuata Aayah zisizo wazi maana yake, basi mjue kuwa hao ndio wale ambao Allaah amewaeleza. Hivyo tahadharini nao.”[5]
Allaah amebainisha kuwa wapotevu wanakusudia fitina:
فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ
“Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotevu hufuata zile zisizokuwa wazi maana zake kutafuta fitina.”
Hutopata mtu wa Bid´ah yeyote isipokuwa utamkuta anafuata Aayah zisizokuwa wazi katika Maneno ya Allaah (Ta´ala), maneno ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au maneno ya wanachuoni ili awapoteze watu kwa hilo. Huu ndio uhakika wa mambo siku zote. Hukuna yeyote aliyepinda kutoka katika mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah isipokuwa anafuata utata huu ili asababishe fitina kati ya watu. Ninamuomba Allaah atujaalie sisi na nyinyi kuweza kufuata Kitabu Chake na kujiepusha na Bid´ah, utata na matamanio.
[1] 06:153
[2] Ahmad (4143). Ahmad Shaakir amesema: ”Mnyororo wake ni Swahiyh.”
[3] al-Bukhaariy (2697) na Muslim (1718).
[4] 03:07
[5] al-Bukhaariy (4547) na Muslim (2665).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 365-366
- Imechapishwa: 19/03/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 365-366
Imechapishwa: 19/03/2017
https://firqatunnajia.com/3-matahadharisho-juu-ya-bidah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)